Habari msomaji wangu, leo ninakuletea Makala hupi inayohusu
utekaji wa mwaka 1998. Utekaji huu ulitokea tarehe 5 mwezi April mwaka 1998,
katika mji wa Cúa, nchini Venezuela, ambapo kijana wa miaka 18 Hector Duarte
Bahamonte alipokwenda kupora katika duka la mikate akiwa na bunduki aina ya
revolver. Mpango wake huo wa utekaji haukufanikiwa, aliamua kuja na mpango
mwingine akamchukua mwanamke mmoja kama mateka wake na kumtishia kumuua.
Maamuzi hayo aliyachukua baada ya polisi kuwasili katika eneo la tukio ambapo
aliwarushia risasi na ushikiriaji huo mateka ulidumu kwa masaa 7. Baadae polisi
waliamua kufanya maamuzi magumu na hapo ndipo skari mmoja kutoka kikosi maalumu
cha polisi akiwa na maski akafyatua risasi ambayo ilimpata Duarte kwenye
kichwa. Duarte alidondoka chini na kupoteza maisha kisha mwanamke mateka akawa
salama. Kifo chake kilinaswa na kamera.
Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa tukio hili lilitokea
katika mji wa Cúa, karibu kilometa 50 kutoka mji wa Caracas kusini, mji
mkuu wa Venezuela. Duarte alipokwenda kufanya upora polisi walipata taarifa na
walifika mara moja kwenye eneo la tukio na kumpiga risasi ya mkono. Mara baada
ya kupigwa risasi ya mkono, Duarte alikimbilia katika nyumba moja ya makazi na
kumteka mwanamke wa miaka 44 aliyeitwa Nancy López pamoja na familia yake.
Duarte aliwafyatulia risasi mateka wawili, mmoja alikuwa mtoto wa kiume wa
miaka 9, na kuwaacha wote wakivuja damu, hapo ilikuwa ni ghorofa ya 9. Kisha
akatoka ndani akiwa na López. Alimuwekea revolver yake kichwani akitishia
kumuua kama hata pata gari la kutorokea. Lengo la Duarte lilikuwa kupata gari
na kukimbilia Caracas. Polisi walianza majadiliano na Duarte wakimshawishi
kumuachia Lopez kisha wapatie gari lakini Duarte hakuwa mwepesi sana. Mkuu wa
polisi Ivan Simonovis ndiye aliyekuwa anaendesha operesheni ya kumuokoa López.
Masaa saba yakakatika, polisi wakiendelea kufanya majadiliano
na Duarte wakimsihi ajisalimishe kwa amani ili kupunguza madhara lakini bado
Duarte hakukubali. Wakati wamajadiiano kati yake na Poilisi, Duarte aliweza
kuongea na mama yake kwa kupitia simu ya polisi. Pamoja na kutishiwa kuuawa
taarifa zinasema, López alikuwa mtulivu sana. Polisi walifanya kila jitihada
kumshawishi Duarte kutatua tatizo lililokuwa linamka bili kwa njia ya amani
lakini alikataa. Sehemu ya ripoti inasema, Duarte alisikika akisema "Mkiniua
na mimi na muua huyu mwanamke. Nipelekeni makaburini mara moja. Leteni majeneza
mawili". Baadae alifika mwanasaikolojia wa jeshi la polisi ambaye
aliendelea na majadiliano na Duarte akiwa karibu na gari moja aina ya van, nyuma
ya van hiyo alikuwepo mlenga shabaha mmoja. Ghafla polisi mmoja aliyekuwa na
maski alifyatua risasi moja akitumia bunduki ya kulengea shabaha yaani sniper
rifle, risasi ilimpata vyema Duarte katika jicho lake la kushoto. Duarte
akadondoka chini na kufariki. Mwanamama Nancy López akawa huru tena akiwa na
mshtuko mkubwa lakini hai.
Duarte alichukuliwa haraka na kukimbizwa kwenye gari la
wagonjwa lakini tayari alikuwa ameaga dunia mara alipopigwa risasi. Lopez
alikimbizwa hospitali japo alikuwa na majeraha machache tu wale mateka wawili
ambao walipigwa risasi nao walipelekwa hospitali. Siku iliyofuata, López
alihojiwa na waandishi wahabari kuhusu tukio lililobaki kidogo kuchukua maisha
yake, alijibu, "Jana nilizaliwa upya; haikuwa siku yangu ya kufa lakini
nilizaliwa upya. Namuomba Mungu ampokee (Duarte) huko juu na kumsaehe maana
mambo yote haya huwa tunafanya pasipokujua kwanini tunafanya na madhara yake,
wacha apumzike kwa amani na amsamehe"
0 Comments