Martin akamtajia nesi yule namba za mkewe
na kisha akampigia simu na kumueleza kuwa afike hospitali ya Mt. Joseph ili
kumuona mumewe.
“Asante sana nesi, unaitwa nani?” Martin
alimshukuru nesi yule na kumuuliza jina lake.
“Usijali ni sadaka tu hii, naitwa Sonia”
Nesi alijibu kuhu akikagua kagua chupa ya drip.
Baada ya muda daktari alifika na
kusalimiana na Martin. “Unajisikiaje?” Daktari aliuliza.
“Najisikia maumivu kiasi katika kichwa,
mkono na mgongo” Martin alimuelezea daktari anavyojihisi.
“Ni sawa, hata hivyo hakuna majeraha
makubwa uliyopata, nimekufanyia vipimo vyote uko salama hakuna mfupa
uliovunjia, uko salama na haya msumivu ni yakawaida kabisa.” Daktari
alimuelezea Martin ambaye alijisikia faraja sana kusikia kuwa hakupata madhara
makubwa kutokana na ajali aliyopata.
Akiwa bado anazungumza na dakari,
Annabelle aliingia akiwa hana hata chembe ya shauku kutaka kujua mmewe
anaendeleaje.
SASA SONGS NAYO..........
“Ooh! Mke wangu, umefika?”
“Hapana naondoka…Kwahiyo hujafa?”
Annabelle aliuliza swali lililowashangaza Martin, nesi na Daktari.
“Mke wangu….” Martin alitaka kusema jambo
lakini mkewe akamkatisha.
“Koma…Nabado huu ni mwanzo tu namshukuru
sana Mungu kwa hili utalipia madhambi yako yote uli….” Annabelle alianza
kubwatuka lakini Daktari alichoka kumvumilia.
“Hey we mama hii ni hospital siyo saluni,
hebu kuwa na ustaarabu basi kama unatofauti na mumeo nenda kamsubiri nyumbani.”
Nesi aling'aka, Annabelle akalielewa somo na taratiibu akaanza kuondoka kuhu
akibinua mdomo. Daktari yule alibaki akimshangaa sana mke wa Martin, naye
Martin alikuwa ameinamisha kichwa chske asijue nini cha kufanya.
Daktari alimgeukia Martin, “Mr. Martin,
hivi huyu ni mkeo kweli?” Daktari alimuuliza Martin.
Martin alivuta pumzi na kuinua kichwa
chake kumtazama Daktari huku akilazimisha tabasamu, “Doctor Rose, naomba
msamaha kwa niaba ya mke wangu kuna tofauti tu za kawaida mme na mke, you know,
so am….”
“It's okey haina haja ya kujieleza sana
nimekuelewa, we endelea kupumzika nadhani jioni nitakuruhusu.” Daktari Rose
alimueleza Martin.
“Asante sana Daktari….”
“Ila kuwa makini na huyo mkeo maana mi
sijapata kuona wanawake wa aina hii aisee kha!”
Martin hakujibu kitu badala yake
alilazimisha tabasamu ila moyoni mwake ni yeye na Mungu wake ndiyo wanajua nini
kilikuwa kinaendelea katika kichwa chake na moyo wake.
“Aah! Nesi am starving naomba unisaidie
kununua chakula…” Martin alimuomba nesi amsaidie kununua chakula baada ya
kuhisi njaa kali.
“Sawa usijali nakuletea.” Nesi alikubali
na kuanza kupiga hakuta kuondoka.
“Subiri nikupatie hela….” Martin alianza
kujipapasa ili atoe pesa lakini hakuwa na pesa yoyote.
“Martin wala usijali we tulia mi
ntakununulia chakula tena kizuri sana, relax babaa”
“Aaah! Asante sana dada angu Mungu
akubariki sana.” Martin alimshukuru nesi. Nesi aliondoka na kwenda kumnunulia
Martin Chakula kisha akamletea. Martin alimshukuru sana nesi kwa moyo wake wa
ukarimu.
Jioni Martin aliruhusiwa na kurejea
nyumbani hakumkuta mkewe alijaribu kumpigia simu lakini hakupokea. Majira ya
saa 3 usiku Annabelle alirejea nyumbani na kumkuta mumewe anamsubiri. “Umetoka
wapi muda huu na kwanini ulikuwa hupokei simu yako?” Martin alimuuliza mkewe.
“Ni nini unachotaka kujua zaidi?” Annabelle
akimuuliza Martin huku akijitupa kwenye sofa.
“Mke wangu sikuelewi, umekuwa na tabia za
ajabu ajabu, kwanini unanifanyia hivi?” Martin alilalamika lakini Annabelle
hakujali hisia za mumewe alisimama na kuanza kuondoka, Martin alimzuia kwa
kutumia fimbo aliyokuwa anaitumia kutembelea ili kuepusha kuumiza mguu wake wa
kulia ambao ulikuwa na maumivu.
“Annabelle hatujamaliza bado, na ni nini
kile ulicholifanya hospitali?”
“Martin hebu niache sawa, sina muda
wakujibizana na wewe nahitaji nikapumzike…” Annabelle alimjibu Martin kisha
akamsukuma akaangukia kwenye sofa, pasi na kujali kama angemuumiza mumewe au
lah. Martin alitikisa kichwa na kumuomba Mungu amsaidie kuwa na moyo wa
uvumilivu.
Martin hakwenda kazini kwa siku kadhaa
kutokana na ajali aliyoipata hivyo aliamua kuwa na mapumziko ya siku kadhaa,
hapo ndipo aliona kila aina ya rangi ambayo hakuiona. Kuna wakati alikuwa
anajiuliza ‘Hivi kweli hii ndiyo aina ya mwanamke nilioa? Hivi huyu ndiye
Annabelle wangu tuliyependana sana? Huyu ndiye Annabelle aliyekuwa anajali na
kuumia nilipoumia, kufurahi nilipofurahi?’ Alizikumbuka zile nyakati nzuri
ambazo walikuwa na furaha pamoja na binti yao, aliumia sana.
Baada ya mapumziko kuisha, Martin alirejea
kazini na kuanza kazi, milango mingi ilifunguka siku hadi siku, akawa hatafuti
wateja ila wateja wanamtafuta yeye.
Siku moja akiwa amekaa na mkewe sebleni huku
kila mtu akiwa na mishe zake, mara simu ya Martin ikaita. Martin akatazama
katika kio cha simu yake akaona ni namba ya mtu anayemfahamu na nimuhimu sana,
akaipokea, “Hallow, habari za mchana chief?” Martin alimsabahi mtu huyo
aliyempigia simu. Lakini kwa kuwa kulikuwa na sauti kubwa ya television
akamuomba mkewe apunguze lakuni mkewe alimpuuza ikabidi afanye hivyo yeye
mwenyewe.
“Ndiyo Chief nakusikia…”
“Mr. Martin, napenda kukupa taarifa kuwa,
kampuni yako imeshinda na nitakupa tutasaini mkataba kesho mchana kutekeleza
mradi wa 3.2 Billions!”
“Chief are you serious? 3.2 Billion! Ooh!
God Bless you, sir.”
Baada ya maongezi hayo Martin aliamua kumfikishia
habari hiyo njema mkewe lakini, mkewe alinyanyuka na kusonya kisha akaingia
chumbani kwake. Hilo Martin alilizoea hivyo kitendo hicho cha mkewe hakikuzuia
furaha aliyokuwa nayo, aliruka ruka na kushangilia.
Siku iliyofuata Martin alikwenda kusign
mkataba wa mabilioni ya pesa. Kutokana na kazi nyingi za siku nzima, Martin
alichelewa kurudi nyumbani lakini alimtaarifu mkewe kwa ujumbe mfupi wa simu
kwakuwa hakupokea simu zake. Hiyo siyo mara ya kwanza kuchelewa kurudi kutokana
na kazi nyingi hata hapo awali alikuwa akichelewa lakini hakuacha kuwa baba na
mume mzuri kwa mtoto wao Ruth na mkewe Annabelle. Baada ya Annabelle kujua kuwa
mmewe atachelewa, alikwenda kwa mlinzi na kuchukua funguo za getini ana
akamueleza mlinzi asiruhusu yeyote kuingia hata kama ni Martin!
Baada ya saa kadhaa Martin alifika,
alipiga honi lakini mlinzi hakufungua, aliamua kumpigia mlinzi lakini
alimueleza kuwa amepewa masharti na mama kuwa asimruhusu mtu yeyote kuingia na
hata funguo amechukua! Martin alishangaa sana, akaamua kumpigia siku mkewe,
lakini kama kawaida mkewe hakupokea simu. Martin aliamua kulala ndani ya gari.
Asubuhi ilipowadia, Annabelle ambaye ni
mke wa Martin, alirejesha funguo kwa mlinzi hivyo Martin akaweza kufunguliwa
mlango na kuingia ndani. Alikasirishwa sana na kitendo cha mkewe, alimfuata
hadi chumbani kwake, “Annabelle nini maana ya hiki ulichokifanya? Yaani kwenye
nyumba yangu mwenyewe, nazuiliwa kuingia, unanilaza nje kwemye gari usiku
kucha, unatatizo gani wewe mwanamke?” Martin alimfokea na kumuuliza mkewe
maswali mfululizo.
“Na bado nitafanya hivyo tena na tena na
tena na tena kwasababu ninakuchukia sana we mwanaume hadi najuta kuolewa na
wewe….!” Annabelle alimjibu Martin, majibu ambayo kamwe Martin hakuweza
kuyavumilia alijikuta amenyanyua mkono wake kutaka kumpiga mkewe lakini
alishangaa kuona na mkewe naye amenyanyua mkono akitaka kijibu mapigo.
“Oooh! Na wewe pia unataka kupigana na
mimi siyo?” Martin alimuuliza mkewe kana kwamba haoni kuwa mkewe kajiandaa kwa
lipi.
“Jaribu uone….” Annabelle alijibu
“Huna maana…” Martin alimuacha mkewe akiwa
amesimama ananesa nesa kama kafungiwa spring miguuni. Martin aliingia chumbani
kwake na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini. Hakumuaga mkewe aliindoka zake
kimya kimya.
Kesho yake Martin hakwenda kazini alibaki
nyumbani akiwaza mambo kadha wa kadha, alitafakari ni kwa namna gani anaweza
kuiokoa ndoa yake. Alisikia kuna watu wanazungumza, aliposikiliza kwa makini
alisikia sauti ya rafiki wa Annabelle. Aliamka kitandani na kutoka taratibu
huku akishuka ngazi kwa umakini.
“Mwenzangu yaani kila siku iendayo kwa
Mungu naona hela zinajaa tu.” Annabelle alikuwa akimwambia rafiki yake aitwaye
Juliet.
“Mimi nakwambia Martin ni mshirikina,
utajiri wake huo siyo utajiri wa kawaida. Kwani hizo pesa anazileta humu
ndani?” Juliet alimueleza Annabelle kama mumewe hutunza pesa ndani.
“Hapana, yaani kila kukicha ni simu za
kupewa tenda za ujenzi ni mabilioni kwa mabilioni yaani hadi naogopa.”
“Shoga yangu sikiliza nikwambie,
ukiendelea kubaki hapa, wewe ndiye utakayefuata kamaliza mtoto anakuja kwako
mama mtoto kuwa makini.” Juliet aliendelea kupigilia msumari.
Martin alishindwa kuvumilia, akaamua
kujitokeza huku akipiga makofi. “Woow Juliet safi sana, kumbe wewe ndiye
unamjaza maneno mke wangu unajifanya kuwa ni rafiki wa mke wangu kumbe huna
lolote ila kuja kuvunja ndoa za watu.” Martin alimwambia Juliet aliyekuwa
kainama kwa aibu.
“Kwani anasema uongo?” Annabelle alidakia.
“Kelele we mwanamke, mwanaume nikiongea
mwanamke unatakiwa kukaa kimya.” Martin alifoka japo maneno yale hakutaka
kuyatumia kumdidimiza mkewe lakini ilimbidi afanye hivyo ili kulinda ndoa yaje
na heshima yake kwa mkewe pia.
“Hivi Martin….” Juliet alitaka kuongea
lakini alikatishwa na sauti nzito ya yenye mamlaka ya Martin.
“Nyamaza kimya, hapa upo kwenye himaya
yangu ninaweza kumufanya chochote kile na hakuna mtu hata mmoja hata marehemu
babu yako akifufuka leo hataweza kunifanya chochote.” Martin alifuwa amefura
kwa hasira.
Juliet aliingiwa na woga wa hali ya juu
huku akiwaza juu ya habari kuwa Martin ni mshirikina, alizidi kuogopa na pia
akafikiri maneno ya Martin na uwezo wa kifedha alionao, hakajuta ni kwanini
alikuja hapo.
“Sasa, hivyo hivyo ulivyo, simama wima,
kushoto geuka hatua tatu mbele kushoto geuka, fungua mlango utoke na usirudi
tena hapa, ione hii nyumba kama kaburi. TOKA NDANI YA NYUMBA YANGU” Martin
alimuamuru Juliet ambaye alitii kila alichoambiwa na Martin. Annabelle pia
alikuwa ameingiwa na woga maana hakuwahi kumuona Martin akiwa amechukia namna
ile. Alihisi baridi na tumbo likiunguruma kwa taratibu kama vile mtu mwenye
njaa.
Baada ya Juliet kuondoka, Martin
alimgeukia mkewe, “Na wewe, fanya vituko vyako vyote lakini nikikuona karibu na
huyu malaya, siku hiyo utataja majina ya wanaukoo wangu wote.” Martin alimuonya
mkewe kisha akarudi chumbani kwake.
Maisha yakawa yanaendelea huku wakiwa kama
chui na paka, hakuna salamu, hapaliki wala hapanyweki. Martin aliamini kuwa ipo
siku lazima mambo hayo yatakwisha. Lakini alitaka zaidi kujua ni nani ambaye
huwa anampa maneno namna ile hadi anazidi kuwa mtu wa ajabu kila kukucha, kila
alipowaza hakupata jibu, aliendelea kumuomba Mungu mambo yaishe mapema maana
amemkumbuka sana mke halisi.
Ilifika siku ya kusherehekea miaka 15 ya
ndoa yao lakini pia ilikuwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Annabelle.
Martin aliamua kumnunulia mkewe zawadi kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa
lakini pia kumshukuru kwa kuwa naye hadi wakati huo japo kuwa alikuwa
anamfanyia vitu visivyo stahili, bado alibaki kuwa mke wa thamani sana kwake na
ndiyo maana alimvumilia kwa kila bala alilomtendea.
USIKOSE SEHEMU YA 5 YA HADITHI HII KESHO




0 Comments