Dakika mbili tatu baadaye, Kombora alikuwa miongoni
mwa polisi wanne waliokuwa katika chumba fulani katika hoteli ya Kilimanjaro.
Chumba hiki kilikuwa cha nne kutoka chumba cha Clay. Hata hivyo, kutokana na
mitambo waliyoitega kitaalamu, japo hawakuwa wakimwona, waliweza kumsikia
anavyoongea katika chombo fulani cha kijasusi.
“Sikiliza mzee… sikia…” askari mmoja alimwambia
Kombora huku akitweta.
“…Ndiyo. Ndiyo… nimefanikiwa kupanda katika majumba ya
kutosha. Moja Ikulu.. hapa Kilimanjaro moja… jengo la IPS moja… Kitegauchumi…
Muhimbili… Benki Kuu ya muda… Tipper… kiwanda cha Urafiki na sehemu mbalimbali
muhimu. Tunachosubiri ni saa moja tu. Ikifika, kwa jinsi nilivyotega inaelekea
jiji zima litalipuka. Mimi nitaondoka hapa wakati wowote…”
“Unasikia mzee?... Unasikia?”
Kombora hakusubiri kumsikiliza afisa huyo. Aliwaamuru
kumfuata kukiendea chumba cha Clay. Kinyume cha mategemeo yao waliukuta mlango
ukiwa wazi. Naye alikuwa kaketi kwa utulivu juu ya kochi, gazeti mkononi. Yeyote
ambaye angeingia bila ya kufahamu kinachotokea angemdhania kuwa alikuwa akisoma
gazeti.
SASA SONGA NAYO...................
Aliwalaki Kombora na wenzake kwa utulivu wa
kushangaza. “Karibuni. Vipi, mbona ghafla hivyo? Kuna habari mpya?” aliuliza.
“Inuka na uweke mikono yako juu,” Kombora alifoka,
tayari akiwa na bastola yake mkononi akiifanya idadi ya bastola zilizomwelekea
kuwa nne.
“Vipi Inspekta! Mbona sielewi?”
“Mikono yako juu!” Kombora alinguruma.
Clay akainuka na kuiweka mikono yake angani.
“Acha gazeti.”
Aliliachia. Ndipo kilipoonekana kikasha kidogo chenye
ukubwa wa kiberiti ambacho alikuwa nacho mkononi. Kombora alimsogelea na
kuiweka bastola kifuani mwake huku akimwuliza kwa ukali, “Nini hicho?”
“Kwa nini Inspekta?... Hiki sikifahamu. Nimekiokota
sasa hivi tu.”
Jibu hilo lilimchukiza Kombora kupita kiasi. Alijibu
kwa pigo zito la ngumi ambalo lilitua barabara katika uso wake. Clay
alipepesuka lakini hakuanguka, jambo ambalo lilimshangaza na kuzidi kumchukiza
Kombora. Pamoja na umri wake mkubwa hakumbuki lini alipata kumpiga mtu ngumi
nzuri kama hiyo na mtu huyo akaendelea kusimama. Akarudi nyuma hatua mbili na
kumwamuru askari mmoja amkague. Ni hapo lilipotukia jambo ambalo
halikutegemewa. Kwa wepesi usio kadirika Clay alichomoa kisu na kumchoma askari
huyo. Kisu cha pili kilimkwaruza Kombora mkononi. Papo hapo alichupa mlangoni
akienda zake. Lakini hakuwa mwepesi zaidi ya risasi tatu za polisi ambazo
zilimfanya aanguke mlangoni kifudifudi. Wakamvuta chumbani na kumlaza kitandani
bila kujali damu zilizoendelea kumtiririka kutokana na majeraha makubwa ya
risasi hizo. Wakamkagua na kumpokonya bastola nyingi na visu sita zaidi.
“Sema haraka, ulikuwa ukiwaarifu nini mabwana zako?”
Kombora alimwuliza.
“Itakusaidia nini Inspekta?” alihoji kwa udhaifu na
maumivu makali. “Huna unaloweza kufanya. Bado saa chache sana. Kama utapenda
kufahamu nilikuwa nikiwaarifu mafanikio ya kazi yangu. Nimefaulu kutega katika
majengo mbalimbali. Wakati utakapowadia mlipuko utakaotokea utakuwa wa
kupendeza sana. Laiti ningekuwa hai nione na kusikia vilio vyenu!” Kombora
hakujua aseme nini. Hakujua kama ilimpasa kumtisha au kumbembeleza mtu huyu
ambaye kila dalili ilionyesha kuwa angekufa haraka. “Mpelekeni hospitali,”
aliamuru.
“Ya nini Inspekta? Sipendi kufa kwa moto… naweza kufa
kwa njia nzuri zaid…”
Kombora hakumsikiliza. Akamgeukia askari wake
aliyekuwa mahututi. Yeye pia hakuwa na dalili ya kuishi sana. Kisu kilimwingia
kifuani upande wa moyo. Jambo hilo lilipandisha hasira za Kombora dhidi ya
Clay. Akamgeukia na kumtazama usoni.
Alimwona akitafuna kitu. Akakumbuka majasusi mengi ya
utawala huo yalivyokuwa yakiishi na sumu kali mdomoni. Matumaini ya kupata
habari zozote za haja yalikuwa mbali. Akamgeukia na kumwuliza taratibu, “Sema
tafadhali… tunawezaje kuzuia mkasa huu ulioko mbele yetu?”
Clay alicheka kwa maumivu huku akijikongoja kusema,
“Labda uchukue furushi moja katika mfuko wangu ukaangalie unachoweza kufanya.”
Moyoni alifahamu kuwa mfuko huo ulikuwa na akiba
nyingine ya vile vigololi, ambavyo alikuwa hajamaliza kuvitega. Hivyo, aliamini
kuwa Kombora angevifikisha Central Police na kulifanya jengo lao liwe moja ya
majengo mengi yatakayopigwa na radi hii iliyoundwa na binadamu. Hilo likamfanya
ajitahidi kucheka, tena kifedhuli huku akisema kwa tabu, “Usijali Inspekta…
muda si mrefu tutakutana huko kuzimu… Tutakuwa wengi sana… mimi natangulia…”
Kombora hakuona kama mtu mwenye roho ya kinyama kama
huyo alistahili kufa kiungwana kiasi hicho. Hivyo, akaichomoa bastola yake na
kumsindikiza akhera kwa risasi ya kichwa ambayo ilimfumua kabisa fuvu lake.
***
Walitazamana kwa macho yaliyojaa hisia. Mmoja
akitabasamu, mwingine akiinama kwa haya. Mmoja akainua mkono wake na kuutua juu
ya paja la mwenziwe. Mwingine akaufunika mkono huo kwa kiganja chake na kuanza
kuutomasatomasa kimahaba. Mkono wa pili ukainuliwa na kutua juu ya kifua cha
mwenziwe, ukitafuta uwezekano wa kupenya, ndani ya mavazi yake. Vijilima
viwili, laini, vilivyosimama kwa namna ya kupendeza macho katika kifua hicho
havikuruhusu mkono huo kupenya kwa urahisi. Mkono ukaviacha vilima hivyo na
kuanza kufungua vifungo vya vazi hilo. Mara kimojawapo cha vilima hivyo
kikajitokeza, kikimeremeta kwa wekundu na uhai wake. Wakatazamana tena. Kisha
akakisogeza kinywa chake na kukifanya kimeze chuchu za kijilima hicho. Mdomo
ulipohama kifuani ulikwenda katika kinywa cha mwingine ambako ulianza kunyonya
ulimi uliokuwa ukisubiri. Mara wakaachana na kuanza kuvua mavazi yao moja baada
ya jingine. Tahamaki wakawa wamesimama kama walivyozaliwa, kila mmoja
akishangazwa au kuridhishwa na uzuri wa mwingine. Kisha wakakumbatiana kwa
nguvu. Mmoja aliguna, mwingine akanong’ona.
“Nuru…”
“Joram…”
Kitanda kikawalaki na kuwafariji. Hawakuhitaji shuka.
Walikuwa kama walivyohitaji kuwa, wakifanya mapenzi kwa namna ambayo
walihitaji, kwa kiwango ambacho hakikadiriki. Vitendo vyao vilifuatiwa na
maneno ya mapenzi ambayo yalisikika kwa sauti ya kike, mara chache sana
yakijibiwa kwa sauti nzito ya kiume.
Kisha ghafla, vitendo na sauti zao vilitoweka machoni
na masikioni mwa mtu ambaye alikuwa akishuhudia kila kitendo chao, “Shit,” mtu
huyo, kwa jina Von Iron, alifoka. Alikuwa akikifuatilia kila kitendo kwa tamaa
kubwa, huku akiburudika. Lakini haikuwa burudani rahisi kwani kuona huko
kulimfanya atetemeke mwili mzima na roho kwa uchu na tamaa, huku jasho
likimtoka na damu kuchemka. Alijaribu kujifariji kwa kuubembeleza uume wake kwa
mkono wake huku macho yake yakiwa yamekazwa kutazama katika mtambo wake. Mkono
haukuwa na faraja yoyote. Mara mbili aliutoa na kuufuta kwa leso yake kwa jinsi
ulivyochafuka kwa manii yaliyomtoka kwa wingi. Alitamani aondoke hapo na kuacha
kutazama vitendo hivyo, lakini macho hayakumruhusu. Akaendelea kutazama,
akiendelea kujifariji kwa mkono wake. Moyo wake ulikuwa unadunda na alishindwa
kustahimili zaidi ya mkono kujifariji. Alihitaji mwananmke. Na si mwanamke
yeyote isipokuwa yule mwanamke aliyekuwa akimtesa sana, mwanamke wa Kiafrika;
Nuru.
Mwanamke mweusi! Von alishangaa kimoyomoyo. Ana
wazimu? Hata hivyo, alijua kimoyomoyo kuwa asingestahimili hadi atakapompata.
Alijifariji kwa kujiambia kuwa angemwua baaada ya kutenda naye mara moja tu,
ili yasije yakampata yaliyompata hayati baba yake.
Ni tamaa hiyo ambayo ilimfanya akatae katakata madai
ya wenzake waliomtaka amruhusu Joram na msichana wake wauawe mara moja.
“Ni jambo la hatari lisilo na busara kumwacha hai mtu
hatari kama huyo hasa katika kipindi hiki,” mwenzake mmoja alimwambia. “Japo
amekimbia kwa na hawezi kurudi, lakini ni mtu ambaye hafai kuaminika. Kumwacha
hai ni sawa na kuishi na nyoka chumba kimoja.”
“Atafanya nini?” Von alikuwa amekanusha. “Hana awezalo
kufanya. Bado saa chache sana tutamleta katika televisheni atazame nchi yake
inavyoteketea. Baada ya hayo tutamchinja kwa urahisi kama kondoo. Usijali.
Waache waishi usiku mmoja zaidi.”
***
Usiku ni kitu alichokuwa akikisubiri kwa hamu,
akikumbuka yale aliyoyaona usiku wa jana. Na ulipowasili hakuwaalika wenzake
kwenda kutazama. Kwa kisingizio cha “Kumchunguza kwa makini.”
Alikwenda peke yake. Akaburudika kwa faraja inayotesa.
Hivyo, vitendo hivyo vilipotoweka machoni mwake, lilikuwa kama pigo kwake.
Aliamini kuwa kulikuwa na hitilafu ya mitambo iliyowaunganisha na chumba hicho.
Lakini kwa kuwa mitambo hiyo ilikuwa automatic, na ilitegeshwa kwa namna ya
kuweza kujirekebisha yenyewe, alisubiri kwa utulivu.
Katika kipindi
hicho cha kusubiri ndipo ilipomjia wazo la kuyafikiria mambo ambayo yangetokea
mara tu baada ya usiku huu. Kesho, wakati kama huu bila shaka nchi kadhaa za
Kiafrika zitakuwa katika maombolezo makubwa huku majeneza yakiwa yamejaa maiti
zilizoungua na hospitali zikishindwa kuhimili idadi ya majeruhi watakaoponea
chupuchupu. Mpango huo uliotokana na ubunifu wake ulipita kwa tabu sana baada
ya wakubwa kulalamika kwamba ulikuwa wa kikatili mno lakini yeye Von na wenzake
wachache walifaulu kuwashawishi na wakaafiki baada ya kuwakumbusha tena na tena
kuwa ANC ilikuwa haifanyi mchezo bali ilikusudia kupokonya utawala, jambo
ambalo lingewatia watu weupe wote mashakani, chama hicho kinapewa onyo kali,
onyo ambalo kamwe lisingeweza kusahauliwa. Dawa ya moto ni moto… na sasa wakati
huo wa kutumia dawa hiyo, iliyokuwa ikichemshwa kwa muda mrefu na gharama kubwa
ulikuwa unawadia. Lipi lingeweza kumpendeza Von zaidi ya hilo? Nani angeweza
kufurahi zaidi yake?
Mara akajisikia kucheka kwa furaha. Alijisikia
kusheherekea kila chozi litakalotoka katika uso mweusi kwani machozi hayo kwake
yangekuwa faraja ambayo isingemsahaulisha ukatili wa mtu mweusi ambaye
alimfanya awe yatima. Maelfu ya weusi yatateketea kwaajili ya malaya mmoja
mweusi, aliwaza. Watakilipia kifo cha mama yake mpendwa, pamoja nao Joram Kiango
na msichana wake… aliendelea kuwaza. Lakini kabla ya kifo chao lazima ampate
huyu msichana anayeitwa Nuru. Aliyoyaona kwa macho yake yalikuwa
hayastahimiliki. Alihitaji kuyaona kwa vitendo. Alihitaji kuijua siri iliyomo
katika ngozi hii nyeusi, siri ambayo ilimfanya amkose mama na baba milele,
baada ya hapo ndipo Nuru angemfata Joram akhera.
Mawazo hayo yalimpandisha mori hata akakumbuka
kuyarejesha macho yake katika screen iliyokuwa ikimwonyesha chumba cha Nuru na
Joram. Hakuona chochote. Mitambo bado ilikuwa haifanyi kazi. Akaitazama saa
yake. Ilikuwa ikikaribia saa kumi za alfajiri. Saa mbili zilikuwa zimepita
tangu mitambo hii ilipokorofisha. Von hakuamini. Isingewezekana kuwa mitambo
hiyo iwe haifanyi kazi kwa muda wote huo ilikuwa imepangwa kuwa ingeweza
kujiwasha yenyewe dakika tano tu baada ya kila hitilafu. Vipi leo ikatae? Na
hasa akiwemo Joram Kiango ambaye, pamoja na matatizo yote aliyokuwa nayo,
iliamriwa asiachwe huru zaidi ya dakika tano?
Hima Von aliinua simu na kuzungusha namba za mmoja wa
makachero waliopewa jukumu la kulala macho katika jumba hilo alimokuwemo Joram.
“Sikia,” Von alimwambia kwa sauti ya amri. “Tumia kisingizio chochote uingie
katika chumba chake humo ndani fanya kila hila uone kwanini mashine hii imegoma
kufanya kazi.”
Akiwa anaijua vizuri kazi yake, mtu huyo alivaa
ovaroli lake jeupe na kuchukua vifaa vya umeme hadi chumbani kwa Joram.
Aligonga mlango kama kawaida. Kisha akagundua kuwa ulikuwa wazi. Akaufungua
polepole na kuingia. Macho yake yalidakwa na umbo la Nuru akiwa kavaa vazi la
kulalia, jepesi kiasi cha kufichua umbo lake zuri la ndani kwa kiwango cha
kutosha. Kando ya Nuru alisimama kijana wa Kizungu aliyevaa nguo zake zote,
suti, kama ambaye alikuwa hajalala kabisa. Fundi huyo bandia alidhani kuwa
kabla ya kubisha hodi mara ya kwanza aliwasikia wakicheka. Lakini hayo
yalimtoka akilini mara alipomwona msichana huyo akiangua kilio huku akisema kwa
kwikwi.
“Afadhali umefika fundi, nadhani utanisaidia.”
“Kuna nini?” kachero huyo aliuliza.
“Huyu hapa,” Nuru alisema akiuelekeza mkono kwa mzungu
aliyesimama kando kwa utulivu. “Huyo ameingia humu chumbani kwa nguvu na kutaka
kuninajisi. Mtoe nje, tafadhali.”
“Yuko wapi bwana wako?”
“Yuko bafuni.”
“Anafanya nini muda wote huo?” fundi bandia aliuliza
huku akizidi kumkodolea Nuru kwa macho yenye tamaa. Mara macho yake yaliuona
mfuko uliokuwa wazi kando ya kabati. Akaona vitu vilivyokuwemo. Aligutuka
kidogo na kurudi nyuma huku akiupeleka mkono wake mgongoni kuchukua bastola
yake. Alikuwa amechelewa sana. Wakati huohuo kisu kilipenya katika kifua chake.
Pigo la pili lilimfanya ateremke sakafuni bila ya ubishi. “Mzungu” aliyekitumia
kisu hicho alikitupa uvunguni na kuifuta mikono yake kwa shuka.
“Fanya haraka Nuru,” alihimiza akiirudia maiti na
kuilaza vizuri kando ya kitanda.
Dakiaka chache baadaye mlinzi aliyekuwa akililinda
jengo hilo kwa mlango wa nyuma aliwaona vijana wawili wazungu, mvulana na
msichana wakimjia. Mikononi walikuwa na mizigo yao ambayo haikuwa chochote
zaidi ya mifuko midogomidogo.
“Tunawahi uwanja wa ndege,” kijana wa kiume alieleza.
Ingawa walizungumza kiingereza kamili lakini mlinzi
huyo alishuku jambo katika sauti hiyo hasa akiwa analifahamu jengo hilo
lilivyo, hakuamini kuwa walikuwa wasafiri wa kawaida.
“Naweza kuona vitambulisho vyenu?”
“Bila shaka,” mwanaume alijibu akiutia mkono wake
mfukoni. Ulitoka na kisu ambacho kilididimia katika kifua cha mlinzi huyo.
Maumivu makali yaliyochanganyika na mshangao vilimfanya afyatue bunduki yake
bila shabaha yoyote. Mara akaanguka chini na kukata roho.
Mlio wa bunduki alfajiri tulivu kama hiyo, uliwashitua
watu wengi. Zaidi yao wote alikuwa Von Iron, aliyekuwa bado kaketi katika
chumba kilekile, akisubiri matokeo ya mtu aliyetumwa chumbani kwa Joram.
Alisubiri kwa muda ambao aliuona mrefu kupindukia. Alipojaribu kuwasiliana naye
kwa walkie talkie ndogo iliyokuwa imevaliwa kama saa ya mkono hakupata majibu
yoyote. Akaendelea kusubiri. Na katika subira hiyo ndipo aliposikia mlio wa
bunduki ambao hakuutegemea. Akafanya hima kumtuma kachero mwingine katika
chumba hicho. Mara moja akapata majibu ambayo yalimfanya atokwe na jasho
jembamba.
Dakika chache baadaye alikuwa miongoni mwa maafisa
sita wa ngazi za juu katika BOSS waliosimama chumbani humo mbele ya maiti ya
mwenzao, ambayo yalilala sakafuni juu ya dimbwi la damu nzito. Joram hakuwemo,
wala msichana wake. Vitu vyao vichache vilikuwa vipo, ingawa baada ya
kupekuliwa havikuonekana na chochote cha haja zaidi ya mavazi na vitabu. Katika
vitabu hivyo kilipatikana kitabu kimoja cha Physics ambacho kilionekana kuwa kilisomwa
sana kwa jinsi kilivyokuwa kimepigiwa mistari chini ya maneno fulanifulani.
Baada ya uchunguzi mdogo ilidhiirika kuwa msomaji alizingatia mambo ya
setilaiti na nyuklia. Hilo liliwafanya waunge mbili na mbili na kupata nne.
“Ana wazimu,” Von alifoka. “Kama amekuja hapa akiwa na
ndoto ya kufahamu chochote juu ya setilaiti yetu hii maalumu wazimu unamsumbua.
Amekuja kuinadi roho yake.” Akawageukia wenzake na kuwatazama kwa lile jicho
lake kali la kutisha, jicho ambalo lilikuwa msingi uliowafanya waendelee
kumwogopa na kutomkosoa. “Mnasikia? Mtafuteni haraka, aletwe hai, atakufa
taratibu kama mbwa wenzake.”
Kabla hawajatawanyika kutoka chumbani humo,
ziliwafikia habari nyingine mbaya zaidi. Maiti ya mmoja wa walinzi wa jengo
hilo imeokotwa ikiwa na kisu kifuani. “Aliuawa kwa aina ya kisu ambacho
kimemwua huyu.” Kachero huyo alieleza.
“Mnaona?” Von
alinguruma. “Sasa namtaka akiwa hai au maiti. Haraka iwezekananvyo, tafadhali…”
Kulitangazwa msako mkali katika jiji la johanesburg
mitaa yote ilifurika makachero ambao walichunguza kila uchochoro. Ilikuwa siku
ngumu mno kwa watumishi weusi ambao walilazimika kuwahi kazini asubuhi hiyo.
Wengi wao waliambulia kuishia katika vituo vya polisi ambako waliteswa na
kusumbuliwa kwa kosa ambalo hawakulifahamu. Mtu au watu waliokuwa wakitafutwa
hawakupatikana. Badala yake hadi mapambazuko kulikuwa na taarifa ya vifo vya
watu wanane zaidi, watano wakiwa wameuwa kwa kisu, watatu kwa risasi za
bastola. Wengi kati ya marehemu hao walikuwa watu wakubwa katika ofisi zao au
walinzi wa majumba fulanifulani yenye umuhimu mkubwa. Ilikuwa dhahiri kuwa hiyo
ilikuwa kazi ya Joram Kiango.
Von alizidi kupandwa na hasira. Hakuelewa kabisa
dhamira na manufaa ya mauaji hayo. “Wazimu unamsumbua,” aliwaza. Kisha alihisi
kuwa ameelewa. Joram alikuwa akilipiza kisasi dhidi ya maafa yatakayoipata nchi
za afrika saa chache baadaye bila shaka alikuwa akijifariji kwa kumwaga damu
zisizo na hatia. “Anajisumbua,” Von alisema. “Atalazimishwa kutazama katika
televisheni, moto utakavyoiteketeza Dar es Salaam. baada ya hapo ndipo
atakapokufa kifo cha kusikitisha…
Von akaamuru ufanyike msako mkubwa zaidi. Polisi wote
na jeshi la ulinzi wakaingizwa katika msako huo. Kila mmoja aliambiwa
anamtafuta nani na afanye nini baada ya kumpata. “Akileta ubishi muue,
vinginevyo mlete hai.”
Ingawa Von alitegemea habari hiyo iwe siri, lakini
hakufahamu iliyafikia vipi masikio ya watu wa habari. Ilimshangaza televisheni
ilipokatiza matangazo yake ya kawaida na kueleza kutoweka kwa Joram Kiango na
mauaji aliyokuwa akiyafanya. Ikatolewa picha ya Joram na msichana wake
walipokuwa wakishuka kutoka ndege iliyowaleta nchini humu ikiwa imetekwa nyara.
Pia zilionyeshwa baadhi ya maiti alizoziua.
“…jihadhari nae, ukimwona muue kwanza, muulize maswali
badaye…”
Mtangazaji wa kipindi hicho alieleza.
Tangazo hilo liliamsha hofu ambayo haikupata kuonekana
katika jiji hilo. Watu walizidi kubababika wakiogopa hata kuifungua milango yao
ilipogongwa na yeyote. Wako ambao kazini hawakutaka kwenda.
Dakika chache baadaye ilibidi Von ajitokeze katika
televisheni na kuwataka wananchi wasiwe na hofu yoyote, kwamba kutoroka kwa
Joram lilikuwa tatizo dogo sana ambalo lingerekebishwa kwa muda mfupi.
Akawafahamisha kuwa badala ya hofu leo ingekuwa siku yao ya kufanya sherehe
kwani Afrika na dunia nzima itaziona nguvu za Afrika Kusini. “Wote ambao
wamekuwa wakionea kijicho na kuitesa nchi yetu leo watatupigia magoti,”
aliendelea. “Tulieni, msiwe na wasiwasi wowote. Ikifika saa nne fungueni redio
na taelevisheni zenu muone…”
***
Watu hao ambao walikuwa wakitafutwa kwa udi na uvumba,
alfajiri iliwakuta wakiwa wamesimama mbele ya hoteli moja ndogo katika mtaa
uliojaa watu waliokuwa wakijadiliana. Macho yao yaliwatazama raia hao wa
makaburu waliojaa wasiwasi kwa dhihaka. Kadhalika, waliwakebehi askari na poli
ambao walikuwa wakipita huku na huko katika mtaa na vichochoro huku wakiwapita
bila ya kuwatupia macho. Isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuwashuku kwa
urahisi. Pamoja na kukesha, pamoja na kuchoka kwa kazi ya kwenda hapa na pale
huku wakilazimika kuua na kuua tena, bado walijitahidi kuwa katika hali ya
kawaida kama raia yeyote wa kawaida katia nchi hiyo. Hali ambao ilitokana na
mavazi waliyovaa pamoja na rangi yao.
Yeyote aliyewaona aliamini kuwa alikuwa akiwaona
vijana wengine wa kikaburu. Hayo yalikuwa matokeo ya moja ya shughuli nyingi
ambazo Joram alifanya kwa gharama kubwa sana aliposafiri hapa na pale katika
miji mbalimbali. Alimpata mtaalamu ambaye aliwatengenezea ngozi za bandia
zilizovaliwa usoni, mikononi na kufunika vichwa vyao kwa nywele za kizungu.
Vitu hivyo ni miongoni mwa mali zake ambazo alizisafirisha kwa hila kwa
kumtumia yule Mmarekani Moole.
ITAENDELEA............................
0 Comments