Filamu kali ambazo Hutakiwi kuzikosa kwa mwaka huu wa 2023

 


Kama wewe ni mpenzi wa filamu, nataka nikwambie kuwa mwaka huu ni mwaka mzuri kwa wapenda filamu kwani kuna filamu nyingi sana nzuri, zenye ubora wa hali ya juu, story nzuri na zitakazoibariki siku yako kila utakapozitazama.

1.       

1. Missing

Filamu inamuhusu Grace (Nia Long) ambaye anakwenda vacation na mpenzi wake lakini anapoteza mawasiliano na watu wake au familia yake. Mtoto wake wa kike, (Storm Reid) anakuwa na jukumu la kumtafuta mama yake kwa kutumia digital footprint. Filamu hii inataka kufanana na filamu iliyotoka 2017 iliyoitwa Searching iliyoongozwa na Aneesh Chaganty. Nakwambia usikose.

Mwongozaji: Nicholas D. Jahnson, Will Merrick

Waigizaji Wakuu: Nia Long, Storm Reid, Amy Landecker

Wasambazi: Sony Pictures

Imetoka: Jan. 20

2.     Knock at the Cabin

Jonathan Groff na Ben Aldridge wanakwenda mapumzikoni na binti yao kisha wanatokea watu wane wasiowafahamu kisha wanaiteka familia hiyo na kuifanya mateka. Hapo ndipo shida inapoanzia.

Mwongozaji: M. Night Shymalan

Waigizaji wakuu: Dave Bautista, Jonathan Groff, Ben Aldridge. Nikki Amuka-Bird, Kristen Cui, Abby Quinn na Rupert Grint

Wasambazaji: Universal Pictures

Imetoka: Feb. 3





3.      2. Creed III

Ni muda wa kurudi tena kwenye ulingo wa ndondi, najua utakuwa ueshaelewa namaanisha nini. Creed ni filamu ambayo imekuwa na mafanikio makubwa sana kwenye soko la filamu duniani na sasa inakuja tena ikiwa inaitwa Creed III ikiwa ni muendelezo wa filamu hii. Filamu hii inakuwa bora sana kwasababu muigizaji Jordan si tu kwamba amecheza kama Adonis bali pia ameongoza filamu hii.

Baada ya kupata nafasi yake katika ulimwengu, ndani nan je ya ulingo, Donnie sasa anapaswa kukabiliana na maisha yake ya nyuma na kujua mambo yote yaliyotokea utotoni mbayo yalimfanya kuwa hivyo alivyo leo.

Filamu hii itatufuchulia kila kitu kupitia kwa mmoja wa marafiki zake wa utotoni na nguli wa zamani wa ndondi, Damian “Dame” Anderson (Jonathan Majors), ambaye anarejea kwenye maisha ya Donnie baada ya kutoka gerezani na anataka kurudisha kila kitu ambacho kilichukuliwa kutoka kwakwe. Kuukabili ukweli ni muhimu Zaidi kwake kuliko ndondi na Donnie atalazimika kupigania kilichochake.

Wakati huu Sylvester Stallon hataonekana kwenye awamu hii na Jordan amekili kuwa anauwezo wa kubeba hadithi ya Creed yeye mwenyewe.

Mwongozaji: Michael B. Jordan

Waigizaji: Michael B. Jordan, Tessa Thompson

Jonathan Majors, Wood Harris, Florian Munteanu na Phylicia Rashad

Wasambazaji: United Artists Releasing

Imetoka: March. 3




4.     3. John Wick: Chapter 4

Baada ya kutamba na filamu hii kwa miaka kadhaa nyuma, sasa Keanu Reeves John anarudi tena kwenye televisheni yako huku akipanga kuishughulikia kikamilifu High Table au bodi ambayo ndiyo inapanga kila kitu kuhusu mauaji na wauaji. Mpango wake huu wa kuisafisha High Table utampelekea kukutana uso kwa uso na marafiki zake wa muda mrefu kama vile Ian McShane’s Wiston.

Kama hiyo haitoshi, mwamba mwingine na mkali wa filamu za mapigano dunianI, Donnie Yen atakuwepo kwenye filamu hii kukupa kila aina ya burudani na kukukumbusha ule uhondo uliowahi kuupata kwenye filamu kama Rogue One na zile harakati zake Hong Kong kama vile Once Upon a Time in China II.

Mwongozaj: Chad Stahelski

Waigizaji wakuu: Keanu Reeves, Ian McShane, Lance Reddick, Clancy Brown, Laurence Fishburne, Bill Skarsgard, Hiroyuki Sanada na Donnie Yen

Wasambazaji: Lionsgate

Inatoka: March 24




5.      4. Fast X

Ukisikia au kusoma jina hili FAST & FURIOUS nadhani kuna picha utakuwa unaipata au siyo? Sasa utakubaliana na mimi kuwa kila toleo jipya la filamu za Fast & Furious huwa kila toleo ni bora kuliko toleo lililopita. Nikutaarifu kuwa unatakiwa kukaa mkao wakula kwasababu FAST X ni habari nyingine kabisaa. Lakini mwisho wa filamu hii utakusikitisha kwasababu ndiyo filamu ya mwisho katika muendelezo wa filamu za FAST & FURIOUS na mwisho wa stori ya Dominic Toretto.

Kama unavyojua kila ingizo jipya linakuwa na adui mpya na adui mpya anapotokea basi ndiyo wakati ambao The Gang wanakutana kumuadabisha.

Kufuatia tukio la mwaka 2021 kwenye F9 Cipher (Charlize Theron) na Dante (Jason Momoa) wanakutana pamoja kwa ajili ya kupambana dhidi ya Dom na kikosi chake ambao wanapata msaada kutoka kwa Tess (Brie Larson). Vipenzi vya mashabiki Vin Diesel, Jason Staham, Michelle Rodriguez, John Cena, Tyrese Gibson, Chris ‘Ludacris’ Bridges, Scott Eastwood, Helen Mirren na Cardi B wanarejea tena na taarifa ni kuwa Rita Moreno naye ataonekana.

Mwongozaji: Louis Leterrir

Waigizaji wakuu: Vin Diesel, Jason Staham, Michelle Rodriguez, John Cena, Tyrese Gibson, Chris ‘Ludacris’ Bridges, Scott Eastwood, Helen Mirren, Charlize Theron, Jason Momoa, Cardi B na Rita Moreno.

Wasambazaji: Universal Picture

Inatoka: May. 19

 

Filamu nyingine kwa kuzitaja tu ni pamoja na The Litter Mermaid imeongozwa na Rob Marshall wasambazaji wa filamu hii ni Walter Disney Pictures. Filamu hii itatoka May 26.

Transformers: Rise of the Beasts imeongozwa na Steven Caple Jr inatoka June 9.

Spider-Man: Across the Spider-Verse Filamu hii imeongozwa na Joaquim Dos Santos, Kemp Powers, Justin K. Thompson Wasambazaji ni Marvels hawana dogo hawa hivyo jipange kupata dozi ya burudani. Filamu hii inatoka June 2.

The Marvels Bonge la filamu, imeongozwa na Nia DaCosta. Filamu hii waigizaji wake si wageni machoni mwa wapenzi wa filamu. Wasambazaji wa filamu hii ni Walt Disney Studios. Inatoka July 28.

Filamu ngingine ambayo sikushauri kuikosa ni hii inaitwa Mission: Impossible – Deas Reckoning Part1. Muongozaji wa filamu hii ni Christopher McQuarrie na miongoni mwa waigizaji ni Tom Cruise mwenye leseni ya kuendesha kila chombo. Wasambazaji ni Paramount na Filamu hii itakujia July 4

Dune: Part Two ni filamu nyingine kali sana ambayo hutakiwi kukosa. Filamu imeongozwa na Denis Villeneuwe. Warner Bros ndiyo wasambazaji ambao wataileta kwako Nov. 3.

Mwezi December tarehe 15 wala haujakaa kinyonge kabisa kwani Warner Bros. Picture watakuletea Wonka kwenye screen ya kifaa chako utakachotumia kutazama filamu zote kali kwa mwaka huu. Mwongozaji ni Paul King.

Post a Comment

0 Comments