ILIPOISHIA.............
Stanley alitulia kidogo na kuvuta pumzi
ndefu kisha kuitoa nje. Alijitengeneza vyema kwenye sofa lenye gharama ya
kununua pikipiki aina ya Boxer kadhaa hivi.
“Uncle, pesa ninayo ya kutosha nikimaliza
nitakwambia.” Akijibu Stanley.
“Sasa kumbe shida nini? Hebu funguka basi
au kam hutaki useme.” Kiasi fulani sauti ya mjomba wake ilionesha kukereka
kutokana na kucheleweshwa kupatiwa habari aliyo ihitaji.
“uncle unakumbuka siku nakwenda kutumikia
jamii nilikupigia simu nikakwambia kuna tukio lilitokea na nikakwambia
nitakueleza nikirudi?” Stanley alianza kufunguka.
SASA SONGA NAYO.............
“Ndiyo! Kwahiyo unabadili mada au ni ile
ile?” Mjomba wake aliuliza huku akijiandaa kuendelea kusoma gazeti lake akijua
wazi kuwa ni kawaida ya Stanley kuanzisha mada mpya kila unapombana akueleze
juu ya kinachomsibu. Stanley hakuwa mtu wakushirikisha mtu mwingine juu ya
matatizo yake, hupenda kupambana mwenyewe hadi atakaposhindwa kabisa ndipo
aombe msaada, hivyo hakushangaa alijua fika kuwa hakuna kilichobadilika kwa
kijana huyo, lakini siku hiyo ilikuwa tofauti.
“Hapana mjomba, wala sibadili mada…...Siku
ile nimetoka hapa nilienda hadi stendi na nikapanda bus nikashuka njiani ili
nipande gari za kwenda kijijini. Lakini dakika kadhaa baada ya kushuka,
walitokea wanaume wawili wakiwa wamejifunika nyuso huku wakiwa na bastola,
walinipora kila kitu na kunibakishia kitambulisho cha uraia tu!” Stanley
alimuelezea mjomba wake kwa masikitiko.
“Mmh! Sasa mbona hukunieleza badala yake
ukanieleza mambo tofauti” Mjomba wake alimshangaa kwa kuwa alikuwa kimya.
Stanley hakujibu kitu, alitulia kama mtu aliyevuta taswira ya jambo fulani,
akatikisa kichwa kusikitika kisha akaendelea, “Hiyo ni cha mtoto, nikijaribu
kuomba msaada lakini hakuna ambaye alinisaidia. Gari kwenda kijijini zote
hazikujubali kunichukua kwakuwa sikuwa na pesa, hata wale wenye gari binafsi
nao walikataa kunichukua.”
“Pole sana uncle, sasa usiwe mnyonge hivyo
uko salama nyumbani au unahitaji msaada wa mtaalamu wa Psychology?” Mjomba wake
Stanley alimuuliza.
“Hapana uncle!” Alijibu Stanley.
“Nini sasa kinakufanya uwe hivyo,
unanitisha.” Mjomba wake alimuuliza huku akimchunguza kwa makini.
“Bado story inaendelea….” Alijibu Stanley
huku akijiweka vyema katika kiti.
“Niliendelea kuwa na subra na hadi
nilipoona gari aina ya Land cruiser VX niaisimamisha. Alikuwa ni familia ya
mume, mke na mtoto wao wa kike. Nilimsalimu na kumueleza yaliyonisibu,
hakuniamini moja kwa moja nikamuonesha kitambulisho akasoma jina langu kisha akashauriana na mkewe na
wakanikubalia nipande ndani ya gari yao.” Stanley aliendelea kumuekeza mjomba
wake.
“Dah!” mjomba wake alishangaa kidogo
“Lakini tukiwa njiani tulivamiwa na
wanaume kadhaa wakiwa na silaha la moto, wakituamuru kushuka kutoka garini,
tulitii. Wakasema wanahitaji mtu kwa ajili ya kafara !” Stanley alisimulia huku
machozi yakimlenga lenga.
“Wait, umesema kafala?” Mjomba wake
alishangaa kusikia hivyo.
“Ndiyo ni kafala…” Akijibu Stanley huku
naye akimshangaa mjomba wake alivyoshangaa.
Stanley aliendelea kumsimulia Mjomba wake,
“Yule baba aliyenipa lift aliwasihi asiumize familia yake na angekuwa tayari
kuwapa kiasi chochote cha fedha ili wasituumize!” Alisita kidogo kusimulia
kisha akaendelea, tayari machozi yalikuwa yameanza kutiririka shavuni.
“Watu wale walikataa wakasema wanahitaji
kichwa cha mtu, yule baba alijitoa yeye ndiyo atumike katika kafara hiyo lakini
watu wale walikataa na waksema wanataka kijana kati ya mimi au binti
yake……Lakini cha ajabu baba yule aliamua kumtoa mwanaye wa pekee na binti yake
mpendwa ili mimi nipone, ilinishangaza sana. Walinchukua binti yule na kuondoka
naye, baba yule alipiga magoti na kulia sana huku mkewe akimlamu kwa kitendo
alichokifanya.!” Sasa Stanley alikuwa anafuta machozi.
“Mmh! Maajabu haya, hadi leo kuna watu
wenye moyo wa namna hii kweli katika hii dunia? Yaani alimtoa binti yake kuokoa
maisha ya stranger?” Mjomba wake alishangaa sana. Kilichomshangaza siyo watu
kutoa kafara ya binadamu ili kupata jambo fulani, bali ni moyo wa mtu huyo
kukubali kumtoa mwanaye wa pekee ili kuokoa maisha ya kijana mwingine ambaye
kakutana naye tu barabarani. Kwa akili ya haraka haraka ya kibinafai sana
angeweza kuruhusu wamchukue kijana huyo ili familia yake iwe salama lakini
badala yake kwanza alijitoa yeye ili familia yake na kijana huyo ambaye kwa
wakati huo ilikuwa ni jukumu lake na iliposhindikana ikabidi amtoe binti yake! Ilimshangaza
sana.
“Kwahiyo huyo jamaa unamfahamu kwa jina au
mahali anapoishi au ulichukua namba zake?” Mjomba wake alimuuliza.
“Hapana uncle na hicho ndicho kinaniumiza
sana” Alijibu Stanley kinyonge sana.
“Dah! Angalau ungekuwa unamjua jina au
mahali anapoishi tungeweza kumtafuta, binti yake hakukutajia jina lake?” Mjomba
we alimuuliza tena.
“Hapana pamoja na maongezi yote tulipokuwa
safarini, sijufikiria kumuuliza jina lake.”
“Stanley, pole sana tuiombee hiyo familia
naamini inapitia wakati mgumu sana.” Mjomba wake alimweleza Stanley ambaye
aliitikia kwa kichwa huku akifuta machozi.
Baada ya wiki moja
kupita Mke wa Stanley alianza kuyazoea maisha ya bila mumewe, alikuwa anajihisi
ni kama mtu aliyetua mzigo mzito aliokuwa ameubeba kwa muda mrefu kutoka safari
ya mbali. Mama yake alikuwa upande wake siku zote kitendo ambacho kingeweza kufanywa
na mzazi yeyote katika zama hizi. Annabelle akiwa amekaa na mama yake,
walisikia mlango ukigongwa, mdogo wake Annabelle aitwaye Dan alienda kufungua
mlango, mgeni hakuwa mtu mwingine bali ni mtu aliyezoea kumuona mara kwa mara,
Martin!
“Karibu shemeji, shikamoo” Dan alimsalimu
Martin bila kinyongo hadi Martin nwenyewe alishangaa.
“Asante, mama nimemkuta?” Martin aliuliza
akiwa bado kasimama nje.
“Ndiyo wapo, pita ndani tafadhali.” Dan
alimkaribisha tena shemeji yake.
Martin aliingia ndani huku akiwa ni mtu
asiyejiamini sana, mara akakutana na macho ya mama mkwe wake! Ni kama moyo wa
Martin uhamie kulia kwa namna alivyostuka.
“Umefuata nini hapa?” Ndiyo sentensi pekee
iliyotoka kinywani mwa Mama Annabelle.
“Shikamoo mama….” Martin msalimu mama mkwe
wake lakini bado mfululizo wa majibu ya kukatisha tamaa na maswali ya kuashiria
kuwa ‘huhitajiki hapa' yaliendelea.
“Mama sijaja kwa shari nimekuja kuzungumza
na wewe pamoja na mke….” Kabla hajamaliza kuongea alikatishwa na Annabelle.
“Ishia hapo hapo, mimi siyo mkeo.” Alijibu
Annabelle kwa hasira.
“Najua unahasira na mimi lakini nawaomba
mnielewe mimi sijamtoa kafara mtoto wangu ili nipate mali.” Martin aliendeleza
ushawishi lakini ni kama kumpigia mbuzi ngoma acheze.
“Ooh! Kwahiyo binti yangu yuko wapi?”
Annabelle alikamuuliza huku amemshikia kiuno.
“Hamuwezi nielewa lakin….”
“Kweli kabisa hatuwezi kukuelewa wala kuku
wa mayai, naomba uondoe kongoro zako hapa na usithubutu kurudi tena hapa…. Toka
ndani kwangu mshirikina mkubwa wewe, unataka unimalizie na mwanangu?” Mama
Annabelle alifoka.
Martin akiona kuwa kwa hali ilivyo hapo,
asiwengeza kusikilizwa badala yake angeishia kuitiwa polisi au kuumizwa,
ilimbidi atii na kuondoka zake.
Stanley mpwa wa Mr. Jerome alikwenda
katika hospitali moja ya serikali ambako rafiki yake wayesoma wote kozi ya
udaktari alikuwa anajitolea katika hospitali hiyo. Lengo likikuwa kuchukua
kitabu chake ambacho alimuazima rafiki yake huyo aitwaye Rahma. Walikutana
katika chumba cha wagonjwa wa dharula, walisalimiana kisha Stanley akamuekeza
kusudi la yeye kuja hapo.
“Ooh! Samahani sana best nimekisahau tena
nyumbani…” Rahma alimueleza Stanley maelezo ambayo yalimfanya anyong'onyee sana
kwani alikuwa anakihitaji sana kitabu hicho.
“Dah! Umenikata moto kabisa mama angu”
“Usiwaze, leo natoka mapema, nitakuletea
nyumbani” Rahma alimuondoa wasiwasi.
“Hapo utakuwa umefanya la mbolea sana.”
Wakiwa katikati ya maongezi, Stanley
aliona binti mmoja anakokota na manesi wawili huku macho yake akiwa kayafumba.
Stanley alihisi kama aliwahi kumuona mahali na ni kama anamfananisha. Alipata
shauku ya kwenda kumtazama kwa makini ili ahakikishe kuwa ni yeye. Naam hakuwa
mbali na kile alichokifikiria, alimtambua binti huyo alipomsogelea karibu,
hakuamini macho yake, aliinua mikono yake juu na kumshukuru MUNGU. Wauguzi
walinahangaa kisha wakaendelea na jukumu lao la kumpeleka binti huyo walipokuwa
wamekusudia kabla ya kusimamishwa na Stanley.
“Hey, vipi unamfahamu huyo binti?” Rahma
aliuliza.
“Ndiyo namfahamu, yuko hapa kwa muda gani
na nini kilimpata?” Stanley alimuuliza Rahma.
“Anamiezi kama sita sasa aliletwa hapa
akiwa hoi alipata ajali ya gari na ni yeye tu ndiye aliyenusurika…. Kwani
unamfahamu vipi huyu binti?” Rahma alimjibu Stanley na kisha kumuuliza swali.
Swali ambalo halikujibiwa, badala yake alimwambia “Asante” kisha akamkumbusha
kuhusu kitabu, baada ya hapo Stanley aliondoka mbio hadi nyumbani anakoishi na
mjomba wake.
Alipofika nyumbani, Stanley hakumkuta
mjomba wake, alisahau kuwa yuko ofisini kwake. Akimpigia simu na kumuomba
amrusuhu kuongea na yeye ofisini kwake. Mjomba wake alimruhusu, Stanley
akaondoka na kuelekea ofisini kwa mjomba wake. Alifika baada ya nusu saa
kwakuwa alikuwa anatumia gani binafsi aliyopewa na Njomba we siku ya sherehe
yake ya kuzaliwa. Afika ofisini kwa mjomba wake. “Nimemwona” Ndilo neno
alilolisema mara tu aliposimama mbele ya mjomb wake.
“Umemuona nani?” Mjomba wake aliuliza.
“Nimemuona yule binti ambaye nilikusimulia
wati ule kuhusu baba yake kuruhusu achukuliwe ili mimi nipone.!” Alijibu
Stanley.
“Una hakika ni yeye?” Mjomba wake
alimuuliza huku naye akiwa na mshangao.
“Uncle ni yeye kabisa….Yupo hospitali ya
Obasanjo mtaa wa Lua!” Alijibu.
“Hebu nipeleke!” Mjomba wake alimwambia na
wakatoka wote ofisini. Waliingia ndani ya gari na kuondoka pamoja kuelekea Lua
Street ambako inapatikana hospitali ya Obasanjo. Ni mwendo wa nusu saa toka
ofisini kwa Mr. Jerome kwa kuwa kulikuwa na foleni kubwa, wakati ambapo hakuna
foleni huwa ni mwendo wa dakika 15 tu.
Baada ya Nusu saa walifika na kuegesha
gari zao yao katika eneo la maegesho ya hospitali hiyo. Walishuka na kuelekea
moja kwa moja mapokezi, walitoa maelezo ya mtu wanayemtafuta na kwakuwa mgonjwa
waliyekuwa wanamuulizia kwa mujibu wa maelezo yao katika hospitali hiyo alikuwa
peke yake. Muuguzi aliyekuwa mapokezi aliwaelekeza kwenda kuonana na daktari
anayemhudumia mgonjwa huyo.
Hawakupoteza muda, moja kwa moja
walielekea katika chumba cha daktari walichoelekezwa, walifika na kuingia tu
pila kugonga hali iliyomstua daktari huyo.
“Mzee vipi mbona unaingia kwa fujo namna
hiyo nini tatizo……” Aliwauliza kwa kufoka.
“Samahani sana Daktari……Ni kama
nakufananisha, wewe siyo Ogbona Ikechuku?” Mjomba we Stanley alimuuliza Daktari
aliyesimama mbele yake.
“Jerome Edochie! Kha! Umenenepa hivi
rafiki yangu unakula vitu gani bwana?” Daktari naye hasira ziliisha baada ya
kumtazama aliyeko mbele yake, alikuwa ni rafiki yake waliyesoma pamoja
sekondari kisha wakapotezana baada ya kila mmoja kwenda A-Level.
Itaendelea............




0 Comments