ILIPOISHIA..........
Maisha yakawa yanaendelea huku wakiwa kama
chui na paka, hakuna salamu, hapaliki wala hapanyweki. Martin aliamini kuwa ipo
siku lazima mambo hayo yatakwisha. Lakini alitaka zaidi kujua ni nani ambaye
huwa anampa maneno namna ile hadi anazidi kuwa mtu wa ajabu kila kukucha, kila
alipowaza hakupata jibu, aliendelea kumuomba Mungu mambo yaishe mapema maana
amemkumbuka sana mke halisi.
Ilifika siku ya kusherehekea miaka 15 ya
ndoa yao lakini pia ilikuwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Annabelle.
Martin aliamua kumnunulia mkewe zawadi kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa
lakini pia kumshukuru kwa kuwa naye hadi wakati huo japo kuwa alikuwa
anamfanyia vitu visivyo stahili, bado alibaki kuwa mke wa thamani sana kwake na
ndiyo maana alimvumilia kwa kila bala alilomtendea.
SASA ENDELEA..........
Aliwahi kurudi siku hiyo hadi mke wake
akashangaa ni kwanini amewahi kurudi namna ile. “Umewahi kurudi mapema hivi
kuna nini?” Annabelle alimuuliza Martin aliyekuwa akimimina mafundo kadhaa ya
maji.
Martin alimtazama mkewe kisha akatabasamu,
“kumbe kuna wakati unajali kuhusu mimi!”
“Sijali chochote nimeuliza tu ili kama
kuna mtu anataka kukuua nimpe ushirikiano.” Annabelle alimjibu mumewe huku
akimimina mvinyo kwenye glass na kuumiminia wote kinywani.
Baada ya dakika chache kupita, simu ya
Martin iliita mkewe akiwa chumbani kwake. Aliipokea, “Hallow boss, tayari ule
mzigo uko hapa” Ilisikika sauti ya mpigaji wa simu.
“Okey, ulishauingiza ndani?” Martin
alimuuliza yule mpigaji wa simu.
“Bado niko nje kabisa boss”
“Sawa, nampa maelekezo mlinzi hapo
atakufungulia geti, uuweke huo mzigo hapo Karibu na huo mti mzuri hapo.”
“Sawa boss.”
Martin alimpigia mlinzi na kumpa maelekezo
ambayo aliyafuata kama alivyoelekezwa.
Martin alikaa kwa dakika kama 10 kisha
akaenda chumbani kwa mkewe kumuamsha.
“Nini wewe unanisumbua mimi nimepumzika,
hebu niache huko”
“Tafadhali mke wangu naomba uongozane na
mimi nina kitu cha kukuonesha.” Martin alimsisitiza sana mkewe.
“Kitu gani?” Aliuliza Annabelle.
“Tafadhali we nifuate mke wangu.”
Annabelle alikubali kumfuata Martin
pengine siku hiyo majini yake yalikuwa yamelala maana alikuwa mpole sana.
Walipofika nje, Martin alimtazama mkewe kisha akamwambia, “Surprise mke wangu,
leo ni kumbukumbu siku ya kuzaliwa kwako nimekupa zawadi ya gari ambayo umekuwa
ukiitaka siku zote na nilikuahidi kukupatia, Range Rover na ile chupa ya
Champaign pale, ni kwa ajili ya kusherehekea miaka 15 ya ndoa yetu…. Happy
Birthday to you honey and Happy anniversary to us!”
Baada ya Martin kuongea Annabelle aligeuka
na kurudi ndani. Martin alibaki akishangaa kuona mkewe hajafurahia, aliamua
kumfuata ndani ili kujua sababu ya kwanini ameondoka bila kusema chochote.
Alifika na kumkuta mkewe ana zunguka
zunguka chumbani huku akionekana kuwa mwenye hasira sana.
“Baby What’s wrong with you, umeondoka kwa
hasira tu nini tatizo?” Martin alimuuliza mkewe ambaye baada ya kumuona mumewe
anaingia chumbani, akasimama akimtazama kana kwamba alikuwa akimsubiria kwa
hamu.
“Ulitegemea nini labda?” Annabelle aliuliza kwa hasira.
“Mke wangu mpenzi nimekununulia zawadi ya
kukupongeza kwa kuongeza mwaka mwingine na pia kukupongeza kwa kuwa umekuwa mke
bora kwangu kwa miaka….”
“Sikiliza Martin sitaki hizo ngonjela
zako, umemuua mwanangu ili upate utajiri. Hongera umefanikiwa lakini nikwambie
jambo moja, sitashiriki katika kutumia pesa haramu, pesa za kishirikina ambazo
umezipata kwa kumuua mwanangu.” Annabelle aliongea kwa uchungu huku machozi
yakimtoka.
“Annabelle unasemaje?” Martin alimuuliza
tena mkewe kana kwamba hakuwa amemsikia vyema.
“Ndiyo wewe ni muuaji, utajiri wako wote
umejaa damu zatu, umekanyaga maiti za watu wengi ili upate utajiri huu, najuta
kuolewa na wewe Muuaji mkubwa.” Annabelle alikuwa amefura kwa hasira lakini
hakujua kuwa Martin alikuwa na hasira na uchungu zaidi yake. Alipomaliza
kuongea alisikia kibao kikali kikipenya katika shavu lake la kulia. Annabelle
alihisi kama anaona giza kisha mwanga halafu giza kisha mwanga, alihisi sikio
lake likipata moto.
“Martin unathubutu kunipiga!” Annabelle
alilalamika kwa mshangao. Hakutarajia kupigwa kibao hicho.
Martin akizinduka kama mtu aliyekuwa
katika ulimwengu mwingibe kabisa. Akijutia uamuzi wake wakumpiga kibao mke wake
kipenzi. Alijutia kushindwa kujizuia na kuruhusu hasira zake zimtawale.
“Mpenzi Samahani….” Martin akimuomba
msamaha mkewe huku akipa magoti.
“Ondoka chumbani kwangu Martin sasa hivi
ondokaaaa”
“Mke wangu Annabelle samahani nimekosea
naomba unisamehe.” Martin aliendelea kumuomba msamaha mkewe huku akiwa amepiga
magoti chini.
“Nasema tokaaaaaaaa!” Annabelle
alipandisha sauti yake juu iliyomfanya Martin atii amri ya mkewe.
Martin alijilaumu sana kwa kitendo kile.
Tangu ameona na mkewe, hajawahi kumpiga kabisa, kitendo kile kilimfadhaisha
sana. Alitoka ndani ya chumba cha mkewe na kwenda kukaa Sebuleni. Alimsikia
mkewe akilia sana lakini kurudi chumbani kwa mkewe haikuwa chaguo bora, aliamua
kutulia.
Annabelle alimpigia simu mama yake na
kumlalamikia kuwa amepigwa na Martin! Mama yake Annabelle hakutaka kuvumilia
kabisa, aliamua kuwapigia simu Baba zake wakubwa na wadogo wa Martin na
kuwaeleza nia yake ya kwenda kumchukua binti yake. Hsikuwa habar njema kwao,
waliamua kumshauri mama yake Annabelle asifanye hivyo badala yake waende wote
kutatua suala hilo. Mama yake Annabelle alikubali ombi la ndugu wa Martin.
Siku iliwadia, kikao cha wanafamilia
kiliandaliwa nyumbani kwa Martin. Baba zake wadogo wawili, baba yake mkubwa
mmoja na wazee wa kimila wawili. Upande wa Annabelle akiwakilishwa na mama yake
tu. Mama yake Annabelle alikuwa ni mtu wa shari sana katika kikao kile aliweza
kuwamudu vyema upande wa Martin, uamuzi wake ulikuwa ni kuondoka na binti yake.
Baba zake wadogo na Martin wakiamua kufanya kazi ya ziada ili kuhakikisha mama
huyo anatulia, walifanikiwa kuntuliza mama Annabelle.
“Mama Annabelle tunaelewa namna
unavyojisikia lakini hebu kuwa mvumilivu, lengo la kikao hiki siyo kuebdeleza
ugomvi bali dhumuni ni kusuluhisha ugomvi wa watoto wetu ili amani na furaha
irejee kama awali.” Mmoja wa baba zake wadogo Martin alimueleza na kumsihi mama
Annabelle apunguze munkali.
“Kwa heshima yako nitatulia lakini….”
“Mmmh! Usisiseme lakini.” Mzee mmoja
ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao kile alimkatisha mama Annabelle. Kisha
akaendelea, “Sasa tumeona picha halisi hapa tuhuma zote zinaelekezwa kwa kijana
wetu Martin……” Mzee yule alisita kidogo kisha akapata fundo moja la maji baridi
kisha akaendelea, “Kwakuwa Martin mwenyewe yuko hapa hebu tumpe nafasi ya
kumsikiliza….” Aliongeza mzee yule na kila nmoja akatikisa kichwa juu chini
ikiashiria kuwa wanaunga mkono hoja yake.
Mzee yule yule ambaye anatokea kijiji
kimoja na alichotoka Martin na ni mtu anayeheshimika sana kijijini kwao.
Alimgeukia Martin, “Martin kijana wangu, tuhuma zote zimekufuata wewe, sasa
nataka utueleze nini kilitokea siku ile….” Alimaliza kumuekeza Martin kisha
akasubiri majibu.
Martin alivuta pumzi ndefu kisha
akawatazama kila mmoja katika kikso kile kisha akaanza, “Awali ya yote
niwashukuru nyote kwa kufika hapa ili kutatua mzozo huu kati yangu na mke wangu
na mama mke wangu.” Martin alitulia tena kisha anaendelea, “Siku hiyo tulianza
safari vizuri kutoka hapa nyumbani kuelekea kujijini kwa aajili ya kusalimia
lakini pia kwa shughuli mbalimbali za kijamii kama kawaida yangu. Tukiwa njiani
tulikutana na kijana mmoja aaliyetusimamisha nasi tukasimama. Kijana yule
alitusalimia mimi na mke wangu kusha akajitambulisha kuwa anaitwa Robert. Baada
ya hapo alitueleza kuwa amepata matatizo, watu wamempora kila kitu chake
ikiwemo fedha zake na nguo alizokuwa nazo.” Martin alitulia tena na kuvuta
pumzi ndefu na kuitoa.
Kisha akaendekea, “Nilimuonea huruma sana,
akatuomba msaada tumfikishe katika kijiji alichokuwa anakwenda kwakuwa nasi
tulimueleza juu ya safari yetu. Pamoja na kumuonea huruma, kuna wakati nilisita
nikidha pengine anaweza kuwa jambazi. Kabla sijatoa maamuzi yangu, ilinibidi
nipate maoni ya mke wangu na mwanangu. Waliafiki tumsaidie na mimi sikuwa na
hiyana nilimruhusu apande garini, alishukuru sana.” Martin aliwaeleza.
Martin alitulia kisha akaendelea
kusimulia, “Kijana yule alionekana kuelewana sana na binti yetu, kama mzazi
ilinipa wasiwasi na niliwaza, pengine anaweza kuwa mtu wanaeelewana sana na
mwanangu tangu muda mrefu lakini kadri walivyokuwa wanazungumza nilibaini kuwa
hawakuwa wanafahamiana. Pia nilikuwa na mawazo anaweza kuwa jambazi, kajini wazo
hili nalo halikuwa na nafasi sana mwisho niliamini kuwa kijana huyo alikuwa mtu
mwema na hakuwa madhara yoyote kwetu.” Martin alitulia, machozi yalianza
kumlenga lenga.
Mzee yule ambaye ndiye kiongozi wa kikao
kile alimwambia ajikaze kisha aendelee kuwasimulia. Martin alijikaza na
kuendelea kuwasimulia. “Tuliendelea na safari yetu ambayo kwa kiasi kikubwa
ilitawaliwa na mazungumzo kati ya binti yangu na kijana huyo, maongezi yao
yakijikita katika elimu na kumcha MUNGU.” Martin aliweka nukta na kufuta machozi
ambayo sasa alishibdwa kuyazuia.
Martin akiendelea kuwaeleza, “Baadae
tulioba gari likitufuatilia jwa nyuma, gali hilo nililitilia shaka baada ya
kusimama na kuziba barabara, tuliendelea mbele kifogo likatokea gari jingine na
kuziba njia kisha wakashuka wati wanne wakiwa na silaha, walituamuru kushuka
garini kisha wakasema wanahitaji kuondoka na mtu mmoja na nilazima awe kijana!
Sikutaka kabisa mtu yeyote adhirike, niliwaomba waiache familia yangu kisha
wanichukue mimi badala yao lakini wakikataa katakata na kusema kuwa wanahitaji
kijana kwa ajili ya kutoa kafala.” Martin alifuta tena machozi na kisha
kuendelea, “Waliendelea kusisitiza na wasema kama nitakuwa msumbufu wataiua
familia yangu, walinipa chaguo kuchagua kati ya yule kijana na binti yangu mpendwa,
Ritha! Hakika ulikuwa wakati mgumu sana katika maisha yangu niliamua kuwaruhusu
wamchukue binti yangu Ritha….” Martin alieleza kwa uchungu huku akiangua kilio
kama mtoto ndogo.
“Mnaona? Niliwaambia huyu ni mshirikina
mkanikatalia. Alimtoa bibti yake mwenyewe kwa ajili ya kafala hapo anajaribu
kutupumbaza tu alipanga kila kitu, sasa sitakubali mwanangu pia awe kafara
nitaondoka na binti yangu.” Mama yake Annabelle alidakia na kupigilia nsumari
wa moto katika moyo wa Martin.
Wazee wake Martin walijikuta wakimuamini
mama yake Annabelle na kushindwa kumuamini kabisa Martin. Kitendo hiki
kilimuuma sana Martin akijaribu kuwaelewesha kadri alivyoweza lakini
ilishindikana. Annabelle alibeba vilago vyake na kuondoka na mama yake japo
kuwa alijitahidi sana kumbembeleza Mkewe (Annabelle) abaki lakini Annabelle
hakuekewa kitu alishikilia uamuzi wake wa kuondoka na kuapa kutomsamehe kamwe.
Martin alibaki chini akiwa haamini
kinachotokea, akiwa bado katika mshangao alisikia sauti, “Bosi…” Ilikuwa sauti
ya mlinzi wake. Alimtazama, alishangaa kumuona akiwa amebeba begi lake,
“Samahani bosi wangu, inabidi niondoke pia” Mlinzi huyo alimueleza Martin.
Martin hakujibu kitu alizidi kushangaa tu
huku akimsindika kwa macho ya mshangao akitokomea katika upeo wa macho yake.
Alisimama na kurejea ndani. Alifika sebleni kwake na kuitazama, aliiona imekuwa
kubwa sana unaweza kugawa hata vyumba vitu na kubaki sehemu kubwa ya sebule.
Machozi yalikuwa yakitoka mfululizo na hayakuwa na kizuizi chochote, alijitupia
kwenye kochi kama gunia la mchele. Kila sehemu aliyoitazama alikuwa akikumbuka
tu namna yeye na familia yake walivyokuwa na furaha. Martin alishindwa kuzuia
uchungu alionao, alilia sana alimlilia MUNGU wake sana.
Ulikuwa ni mwanzo
wa machungu kwa Martin, taarifa zilizagaa kuwa, “Millionaire Martin Okafor ni
mshirikina.” Taarifa hizi zilimuumiza lakini hakutaka kupambana nazo kwakuwa
alijua fika hata afanye nini kwa uwezo wake hatoweza zaidi sana atajikuta
akitenda dhambi ambayo itahalalisha uvumi huo. Alijisemea, “Vita hivi nakuachia
eeh Mungu, naomba unishindie.”
Stanley Ikena kijana ambaye kwa mara ya
kwanza katika maidha yake alijikuta akiandamwa na matukio mfululizo. Kwanza
ilikuwa siku ile alipokuwa anasafiri kutoka jeshini kwenda kijijini kwso
kutumilia jamii kwa mwaka mmoja, akiwa anasubiri usafiri aliporwa kila kitu
chake. Haikuishia hapo, lilitokea tukio jingine baya na lililomuachia
kumbukumbu ya kufundisha, kushangaza na kusikitisha. Tukio hili lilimkosesha
raha sana. Alirudi kwa mjomba wake aitwaye Mr. Jerome ambaye ni mfanyabiashara
mkubwa tu jijini Lagos.
Siku moja Stanley aliamua kumueleza mjomba
wake juu ya tukio zima lililotokea siku ile alipoaga kuwa anakwenda kutumikia
jamii kijijini kwao. Alikwenda Seating room na kumkuta mjomba wake akijisomea
gazeti.
“Shikamo mjomba.” Stanley alimsalimia.
“Ooh! Stanley, marahaba uncle kumbe
ulikuwepo ndani?” Aliitikia Mr. Jerome.
“Ndiyo sijaenda chuo leo!” Stanley
alimueleza mjomba wake.
“Kwanini, unaumwa?” Mjomba wake alimuuliza
huku akiacha kusoma gazeti lake.
“Hapana uncle, kuna kitu kinanisumbua tu?”
Stanley alijibu kinyonge sana hali iliyomfanya Mjomba wake awe na wasiwasi.
“Au umemaliza pesa?” Mjomba wake
aliendelea kumdadisi.
Stanley alitulia kidogo na kuvuta pumzi
ndefu kisha kuitoa nje. Alijitengeneza vyema kwenye sofa lenye gharama ya
kununua pikipiki aina ya Boxer kadhaa hivi.
“Uncle, pesa ninayo ya kutosha nikimaliza
nitakwambia.” Akijibu Stanley.
“Sasa kumbe shida nini? Hebu funguka basi
au kam hutaki useme.” Kiasi fulani sauti ya mjomba wake ilionesha kukereka
kutokana na kucheleweshwa kupatiwa habari aliyo ihitaji.
“uncle unakumbuka siku nakwenda kutumikia
jamii nilikupigia simu nikakwambia kuna tukio lilitokea na nikakwambia
nitakueleza nikirudi?” Stanley alianza kufunguka.
USIKOSE KUFUATILIA HADITHI HII YA JARIBU LA USHINDI SIKU YA JUMANNE.
0 Comments