ILIPOISHIA............
Annabelle alipoamka alikuta kiasi cha pesa
cha shilingi milioni 3 tofauti na ilivyokuwa awali kuwa kila mwisho wa mwezi
hupewa milioni 2. Alizichukua zote na kuziweka katika kisanduku chake ambacho
hukitumia kuhifadhi pesa zake. Alijiandaa na kisha akachukua ufunguo wa gari
lake aina ya Benz na kuondoka kuelekea kwa rafiki yake aitwaye Juliet.
Walipoonana
walikumbatiana kwa kuwa hawakuwa wamekutana kwa muda mrefu sana.
Walianza maongezi yao na Annabelle
akamueleza rafiki yake kila kitu juu ya kile kilichotokea hadi mtoto wao
akauawa. Juliet alimpa pole rafiki yake na kumshauri kukaa mbali na Martin
kwani kuna uwezekano akamuua pia ili ajipatie utajiri, maneno yale yalimuingia
Annabelle na akayabeba kama yalivyo.
Anabelle aliporudi nyumbani alianza kutafakari juu ya mambo ambayo aliambiwa na rafiki yake naye alihisi kuwa ni kweli kwa kila kitu alichoambiwa na rafiki yake, hapo hasira na chuki dhidi ya Mumewe iliongezeka.
SASA ENDELEA..........
Njioni mumewe alirejea akiwa na hamu sana
na mkewe lakini hakujua ni kwa namna gani mkewe alivyo jazwa sumu. Alifika na
kukuta mkewe amelala tofauti na alivyozoea akitazama television. Alienda kuoga
na kisha akarejea sebleni, alikaa kwa muda kidogo kisha akanyanyuka na kwenda
chumba alicholala mkewe. Alipofika alikuta mkewe amelala kihasara hasara,
akahisi damu inamchemka kuliko kawaida, mapigo ya moyo wake yakaanza kumwenda
mbio mbio, jogoo la mjini likawika shamba. Martin akamsogelea mkewe pale
kitandani na kuanza kumpapasa mkewe mapajani taratibu mkono wake ukielekea kibo
na mawenzi, akiwa anakaribia kibo mara mkewe akastuka alipomuona mumewe
alimsukuma kwangu. Martin akadondoka chini!
“Honey nini hiki sasa?” Martin alimuuliza
mkewe kwa mshangao.
“Nini kuhusu nini?” Annabelle naye akajibu
kwa swali huku akiwa amefura kwa hasira.
“Baby kwanini unaninyima haki yangu?”
“Haki ipi? Nakuuliza wewe muuaji haki
ipi?”
“Annabelle wewe ni mke wangu tena wa ndoa
na hii ni haki yangu unaninyima kwa miezi mitano sasa why are you doing this to
me?” Martin alimlalamikia mke wake.
“Mke! Haki! Hivi unadhani kwa kwa kile
ulichokifanya kwa mtoto wetu bado unayo haki juu yangu? Hapana Martin, huna
haki hiyo tena na kwa taarifa yako, huu ni mwanzo tu, utateseka sana.”
Annabelle alimueleza mumewe maneno ambayo kwa hakika yalimuumiza sana Martin.
Baada ya kumueleza maneno yale Annabelle akachukua mto mmoja kwenda kulala
chumba cha wageni. Hili hakulitegemea japo anaelewa wazi kuwa mkewe huyo
anamchukia sana lakini hadi kulala vyumba tofauti, hii ilimuwashia taa ya
kijani, hakutaka kumzuia alimuacha kisha akarejea kitandani. Alitazama kaptula
yake tayari ilikuwa inaunyevu unyevu sehemu ya mbele, akatikisa kichwa kisha
akachukua taulo yake na kuingia bafuni kuoga, alipomaliza alijiweka sawa kisha
akalala.
Asubuhi ikafika Martin alijiandaa kwa
ajili ya kuelekea kazini, alipofika mlangoni alikumbuka kuwa yeye na mkewe
hawakulala chumba kimoja, hivyo akaamua kwenda kumjulia hali mkewe, aligonga
mlango lakini hakujibiwa aliamua kuufungua. Akiingia ndani ya chumba kile na
kukuta mkewe yuko kwenye usingizi mzito huku akijigeuza kuelekea upande
mwingine, Martin alitabasamu kisha akaufunga mlango na kuelekea kazini.
Annabelle alipoamka alijiandalia kifungua
kinywa kisha akakumbuka kumpigia mama yake simu. Mama yake alipokea na
kumuuliza anaendeleaje.
“Mama naendelea vizuri ila namkumbuka tu
mwanangu mama….” Annabelle alianza kulia wakati akimuelezea juu ya hali yake na
namna alivyomkumbuka Ruth.
“Mwanangu, Juliet ameniambia kila kitu ni
kwanini hukuniambia mapema…. Huyo mwanaume inaonekana wazi ni mshirikina, hizo
mali ni kwasababu ya kutoa watu kafara sasa ameamua hadi kumtoa kafara mtoto
wake mwenyewe, unbelievable!”
“Mama ninaumia sana kwa kweli, mtoto
mwenyewe alikuwa mmoja kama dawa halafu kirahisi rahisi tu anakufa jamanii
mamaaa.” Annabelle aliendelea kumueleza mama yake kwa uchungu.
“Pole mwanangu, usijali I've to do
something before it's too late….Usijali mwanangu ila naomba uwe makini sana na
huyo mwanaume.”
“Sawa mama nitakuwa makini sana.”
Annabelle alimaliza kuongea na mama yake
na kisha wakakata simu.
Mama yake Annabelle aliamua kumpigia simu
Martin na kuanza kumtukana na kumtuhumu kuwa amemuua mjukuu wake, Martin
akijitetea sana lakini hakuna kitu kilichobadilika, mama mkwe huyo aliendelea
kumtuhumu kuwa mali zote alizonazo ni kwa sababu alitoa kafara ya watu ili awe
tajiri. Hii ilimuumiza sana Martin aliamua kukata simu. Alitaka kupata msaada
kutoka kwa mtu, na mtu pekee aliyemfikiria alikuwa ni Juliet!
Alichukua funguo za gari na kutoka katika
ofisi yake huku akimuelekeza secretary wake kukata mikutano yote aliyokuwa nayo
siku hiyo na kuipangia tarehe nyingine.
Aliingia ndani ya gari yake na kuelekea anakofanyia kazi Juliet katika
kampuni ya simu ya MTN.
Juliet alikuwa nje ya jengo la makao makuu
ya kampuni ya simu ya MTN, alikuwa akizungumza na mtu mara akaja kijana mmoja
ambaye alimueleza kuwa kuna mtu amemuagiza amuite.
“Ni nani?” Juliet alihoji kwa mshangao.
“Simfahamu…Yuko pale kwenye maegesho ya
gari.”
“Okey asante…. Naomba uniwie radhi, ngoja
nikamuone huyo mtu.” Juliet alikubali wito kisha akamuaga mtu akiyekuwa
anazungumza naye na kwenda kumuona mtu aliyeelekezwa kuwa yuko kwenye maegesho
ya magari.
Juliet alipofika hakuamini, alikuwa ni Martin,
mume wa Annabelle. Hasira zikamjaa, “Unafanya nini hapa?” Juliet alimuuliza
Martin kwa hasira.
“Juliet salamu kwanza basi…”
“Hakuna haja ya salamu…. Sikia sema shida
yako na uondoke!”
Martin alibaki akidua maana Juliet akiyeko
mbele yake muda huo si Juliet yule aliyekuwa akimchangamkia na kumsifia kila
wakipokutana. “Anyway, Juliet niko hapa kukuomba msaada!”
“Wa kumuua Annabelle?” Juliet alimuuliza
Martin swali gumu na la ajabu sana.
“WHAT?” Martin aliuliza kwa shangao
hakuamini alichokisikia kutoka kwa Juliet.
“Ooh! Ulidhani siri yako haitafichuka eeh?
Ulidhani hatutajua kuwa wewe ndiye uliyemtoa kafara mwanao mwenyewe ili upate
utajiri ulionao sasa na sasa unataka umuue na 7 yangu,hapo umekwama Martin.”
Juliet aliongea maneno makavu makavu ambayo yalimduwaza Martin.
“Excuse Me! Juliet, what the hell are you
talking about?” Martin aliuliza kwa mshangao.
“Martin, sina muda wa kupoteza na Wewe,
kusanya makongoro yako na uondoke hapa sasa hivi…”
“Juli…”
“Martin ondoka haraka au nitaita walinzi,
muuaji mkubwa wewe.”
Martin hakuwa na la kufanya aliamua
kuingia ndani ya gari yake na kuondoka huku akiwa na machungu moyoni na
kichwani mwake maneno kama kafara, muuaji yalizidi kujirudia kichwani mwake.
Martin alijikuta machozi yakimtoka, akaanza kulia kwa uchungu huku akimuuliza
Mungu kama kweli yeye ni mbaya kiasi hicho. Akiwa kwenye dimbwi la mawazo mala
bodaboda akakatiza mbele ya gari yake haraka akaanza kumkwepa na bahati mbaya
akaenda kuigonga nguzo ya umeme iliyokuwa upande wa kulia, akazimia hapo hapo.
Martin alipoamka alijikuta yuko juu ya
kitanda cha hospitali, alipotazama pembeni yake kulikuwa na chupa ya drip,
alipojitazama akaona amefungwa budge maeneo mbali mbali ikiwemo kichwani.
Alipotazama mlangoni alimuona nesi akiingia.
“Taratibu utajiumiza, tulia tu acha
kuhangaika” Ilikuwa ni sauti ya upole ya nesi.
“Nimefikaje hapa nini kimetokea?” Martin
aliuliza kwa shida kwa kuwa alikuwa anahisi maumivu sehemu mbalimbali za mwili
wake.
“Umeletwa hapa na waaamaria wema, ulipata
ajali ya gari!”
“Ooh! My God nimekumbuka…Daktari yuko
wapi?” Martin alimuuliza yule nesi.
“Usijali daktari atafika muda si mrefu.”
Nesi alijibu kwa sauti ya kiungwana sana iliyomvutia Martin hata kutamani
aendelee kukaa hapo hospitali.
“Je, kuna mtu yeyote ungetaka kuwasiliana
naye kumueleza juu ya hali yako?” Nesi alimuukiza Martin.
“Yeah yupo, simu yangu….”
“Hakuna simu iliyoletwa hapa pengine….”
“Wameshaiba wasamaria wema” Martin alijibu
kimasihara hadi nesi akajikuta amecheka kama ni mazuri.
“Unavituko sana wewe, usijali nipatie
namba za mkeo nimpigie”
Martin akamtajia nesi yule namba za mkewe
na kisha akampigia simu na kumueleza kuwa afike hospitali ya Mt. Joseph ili
kumuona mumewe.
“Asante sana nesi, unaitwa nani?” Martin
alimshukuru nesi yule na kumuuliza jina lake.
“Usijali ni sadaka tu hii, naitwa Sonia”
Nesi alijibu kuhu akikagua kagua chupa ya drip.
Baada ya muda daktari alifika na
kusalimiana na Martin. “Unajisikiaje?” Daktari aliuliza.
“Najisikia maumivu kiasi katika kichwa,
mkono na mgongo” Martin alimuelezea daktari anavyojihisi.
“Ni sawa, hata hivyo hakuna majeraha
makubwa uliyopata, nimekufanyia vipimo vyote uko salama hakuna mfupa
uliovunjia, uko salama na haya msumivu ni yakawaida kabisa.” Daktari
alimuelezea Martin ambaye alijisikia faraja sana kusikia kuwa hakupata madhara
makubwa kutokana na ajali aliyopata.
Akiwa bado anazungumza na dakari,
Annabelle aliingia akiwa hana hata chembe ya shauku kutaka kujua mmewe
anaendeleaje.
“Ooh! Mke wangu, umefika?”
“Hapana naondoka…Kwahiyo hujafa?”
Annabelle aliuliza swali lililowashangaza Martin, nesi na Daktari.
0 Comments