ILIPO ISHIA.........................
“Baba leo utanipeleka cinema?” Ritha
alimuuliza baba yake ikiwa ni ahadi aliyopewa na baba yake kabla hajafanya
mtihani wa taifa.
“Oooh! Yeah lazima twende na umwambie mama
yako leo ajiandae leo usiku tutakwenda Cinema kuna filamu mpya ya Ken Eric na
Yul Edochie waigizaji mnaowapenda”
“Asante baba, nakupenda”
“Nakupenda pia mwanangu” Martin naye
alijibu na kumuacha binti yake aende kwa mama yake.
Martin alimuwekea utaratibu binti yake
kuwa endapo anataka vitu vya kujifurahisha ni lazima avifanyie kazi, hawezi
kuvipata bure tu. Hivyo ndivyo ilivyotekea kabla hajafanya mtihani, Ritha
alimuomba baba yake ampeleke kwenye Cinema lakini baba yake alimwambia kuwa
utaratibu ni ule ule, nilazima afaulu mtihani kwake ndipo anpekeke Cinema.
Utaratibu huu ulimsaidia sana Ritha kufanya vizuri shuleni kwani alijua
kwakufanya hivyo basi angepata chochote anachotaka bila maswali.
Alipofika kidato cha tatu alipata likizo
ya katikati ya mwaka yaani nusu muhula ambapo awali aliahidiwa akifaulu basi
atapelekwa kijijini kupumzika na babu na bibi yake jambo ambalo Ritha alikuwa
analisubiria sana.
Siku ya safari iliwadia, na siku hiyo
ilikuwa ni mwisho wa wiki yaani jumamosi, walidamka asubuhi na mapema kila
mmoja akajiandaa kwa ajili ya safari. Waliingia ndani ya gari yao na kuanza
safari kuelekea kijijini kwao.
SASA ENDELEA.............
Ninabell alianza kumchukia sana mume wake
kwasababu ya kifo cha binti yao, Ruth. Martin alijitahidi kuomba msamaha kadri
alivyoweza lakini ilishindikana, aliamua kumpa muda mkewe akiamini pengine ni
kwasababu anapitia wati mgumu sana tika maisha yake baada ya kumpoteza binti
yao kipenzi. Martin aliamua kuwa imara kwa ajili ya mkewe na hata yeye pia japo
ndani ya moyo wake alikuwa na maumivu makali sana kwa kifo cha binti yao
mpendwa. Juna wakati alikuwa akikaa ofisini huinamia meza yake na kuanza kulia
kwa uchungu aliokuwa nao lakini akiwa na mkewe au watu wengine, huwa
anajionesha kama mtu imara na asiye na asiye na maumivu au majuto yoyote na hii
ndiyo ilikuwa sababu ya mkewe kuzidisha chuki dhidi yake.
Baada ya miezi mitatu kupita Martin
aliamua kufanya kazi kwa bidii na alimuomba Mungu sana amsamehe na amtie nguvu
katika kufanya kazi zake pengine mafanikio yangeweza kumfanya mkewe angalau
apoteze mawazo na aanze kujivunia kuwa na mwanaume imara.
Siku moja asubuhi na mapema ikiwa ni
mwanzo wa wiki, Martin alidamka kama kawaida yake alijiandaa kwa ajili ya
kuelekea kazini. Alifika mezani na kukuta meza nyeupe, alimuita mkewe aliyekuwa
anatazama picha ya binti yao, “Mke wangu…Mke wangu…. Annabelle si ninakuita!”
Mkewe alintazama na kisha akaendelea
kutazama picha, Martin alianza kupandwa na hasira kidogo kutokana na dharau
aliyooneshewa na mkewe. “Annabelle kwanini hujaniandalia chai wakati unajua
kabisa kuwa huwa nakunywa chai nyumbani kabla sijaenda kazini?” Martin alimuuliza
mkewe kwa sauti ya ukali kidogo.
“Eeeeh! Ishia hapo hapo muuaji mkubwa
wewe….Kimya, kwani jiko hulioni lilipo?” Annabelle alimjibu mumewe ambaye
alibaki akidua kwa maneno ya mkewe.
“Annabelle! Ni wewe mke wangu unayasema
haya?” Martin hakuamini kabisa alichokisikia lakini huo ndiyo ukweli kuwa mkewe
alikuwa amebadilika sana, ilimuumiza sana hali hiyo lakini aliendelea
kujitahidi kumuelewa mkewe kuwa bado anawati mgumu. Aliamua kubeba begi lake la
kazini na kuondoka.
Martin alifika kazini baada ya dakika 20
na hakika na kuketi katika kiti chake. Alianza kutafakari mambo yaliyotokea
nyumbani kwake mapema asubuhi, aliumia sana, alisikia sauti ndani mwake
inamwambia, ‘You are not a Victim but a victor.’ Alistuka na kuketi vizuri
kwenye kiti chake cha kiboss ofisini kwake, kisha akatabasamu. Akiwa bado
katika tabasamu akasikia simu yake ya mezani inaita, akaipokea haraka, “Hallo,
Mr. Martin hapa….”
“Ooh! Habari, unaongea na Dkt. Egube Ike,
nimekupigia kukutaarufu kuwa niko tayari kufanya kazi na wewe na kwa kuanza
nitakupatia mradi wa 2.5 Billion nahitaji mradi ukamilike kwa haraka sana.”
“Sir, are you serious?” Martin aliuliza kqa mshangao kwakuwa hakutarajia alichokisikia kwenye simu hiyo. Alifurahi na kumshukuru sana Dkt. Egube. Alimuita secretary wake na kumpa maelekezo na mara moja kazi ikaanza.
Jioni alirudi nyumbani akiwa hoi na njaa
pia, alimkuta mkewe anatazama television, alimsalimu mkewe lakini aliambulia
msonyo wa karne akajiongeza mwenyewe kimya kimya hadi mezani ambako nako
hakukuta chakula chochote licha ya kuacha pesa za kutosha. Alidhani pengine
chakula kipo jikoni, alipofika alikuta kulikuwa na dalili kuwa kulipikwa lakini
hakuna kilichobaki kwa ajili yake! Alitaka kwenda kumuuliza mkewe lakini akaona
haitakuwa sawa kufanya hivyo na itasababisha ugomvi kitu ambacho hakutaka
kitokee.
Alirudi sebleni ambako alichukua kibegi
chake na kuingia ndani, akijitupa kitandani taratibu usingizi ukaanza
kumnyemelea, hajutaka hilo litokee mapema hivyo, alioga na kisha kubadili nguo.
Akachukua funguo za gari lake na kuelekea nje alikolipaki, aliingia na kisha
kuondoka taratibu, akakamata barabara iliyokuwa inaelekea mjini huku
akisikiliza mziki wa injili toka kwa msanii maarufu nchini Nigeria. Alifika
kwenye mataa na kusimama baada ya taa nyekundu kuwaka, baada ya dakika kama
moja taa ya kijani iliwaka naye akaweka gia ya kuondokea na kupinda kushoto
hadi katika mgahawa maarufu F&J restaurant, mgahawa unaomilikiwa na ndugu
wawili, aliagiza chalula apendacho na kisha baada ya dakika kadhaa akiwa
anaendelea kula aliagiza chakula kingine kwa ajili ya mkewe, japo jikoni
kulikuwa kuna dalili kuwa kulipikwa, aliamini pengine mkewe alimpikia mlinzi.
Alibeba kile chakula na kurejea nyumbani
kwake, akimkuta mkewe bado anatazama television, hakutaka kuongea nae maneno
mengi sana, akimuekea kile chakula mezani na kumwambia, “Mke wangu chakula
chako kiko hapa mezani, usiku mwema.”
Mkewe wala hakujibu kitu na Martin
alilizoea hilo kutoka kwa mkewe hivyo hakujisumbua sana.
Aliingia kulala na baada ya muda mkewe
aliingia chumbani. Martin alikumbuka kuwa kuna habari njema hajamueleza mkewe
hivyo ikabidi amueleze, “Mke wangu nimekumbuka kitu, leo nimepata contract ya
2.5 Billions…Mungu amekuwa mwema sana kwetu.” Martin alimueleza mkewe lakini
badala yake alipokea msonyo ule ule wa karne kisha mkewe akavuta shuka lake na
kugeukia ukutani.
Asubuhi Martin mtu wa kazi aliamka na kama
kawaida yake alijiandaa na kupita mezani lakini hakukuta chochote akaendelea na
safari yake kuelekea kazini hakutaka kumuamsha mkewe alimuachia fedha kwa ajili
ya chakula na matumizi yake binafsi ikiwa ni kawaida yake kumpa mkewe kila
mwezi kiasi cha million 2 kwa ajili ya matumizi yake binafsi kwa kuwa hafanyi
kazi na alikataa kufanya kazi mara baada ya kumpoteza mtoto wao kwa madai kuwa
anahitaji muda ili awe sawa.
Annabelle alipoamka alikuta kiasi cha pesa
cha shilingi milioni 3 tofauti na ilivyokuwa awali kuwa kila mwisho wa mwezi
hupewa milioni 2. Alizichukua zote na kuziweka katika kisanduku chake ambacho
hukitumia kuhifadhi pesa zake. Alijiandaa na kisha akachukua ufunguo wa gari
lake aina ya Benz na kuondoka kuelekea kwa rafiki yake aitwaye Juliet.
Walipoonana
walikumbatiana kwa kuwa hawakuwa wamekutana kwa muda mrefu sana.
Walianza maongezi yao na Annabelle
akamueleza rafiki yake kila kitu juu ya kile kilichotokea hadi mtoto wao
akauawa. Juliet alimpa pole rafiki yake na kumshauri kukaa mbali na Martin
kwani kuna uwezekano akamuua pia ili ajipatie utajiri, maneno yale yalimuingia
Annabelle na akayabeba kama yalivyo.
Anabelle aliporudi nyumbani alianza
kutafakari juu ya mambo ambayo aliambiwa na rafiki yake naye alihisi kuwa ni
kweli kwa kila kitu alichoambiwa na rafiki yake, hapo hasira na chuki dhidi ya
Mumewe iliongezeka.
ITAENDELEA...........
_________________
0 Comments