Jamaa mmoja kwa jina la Martin Okafor
aliyetokea katika familia duni, alifanikiwa kumaliza elimu ya msingi kwa taabu
na kufaulu vizuri kisha akaenda Sekondari kwa msaada wakanisa, ambako alifanya
vizuri sana. Kanisa lilimfadhili katika elimu ya juu ambako alifaulu na kuwa
msanifu majengo. Alifanya kazi kwa muda wa miaka kumi katika kampuni moja na
baadae nwajiri wake alifurahishwa sana na nidhamu, kujituma kwake, uaminifu
wake, namna alivyoongoza wenzake, ucha MUNGU. Siku moja alimuita ofisini kwake,
“Naam bosi nimesikia unaniita.” Martin aliitikia wito wa bosi wake.
“Ndiyo Martin, unaendeleaje na kazi?” Bosi
wake mzee wa miaka 70 lakini ukimtazama ubaweza sema anamiaka 45 tu!
“Salama tu bosi, mafanikio ni makubwa.”
Akijibu Martin huku akionesha tabasamu lake ambalo mara nyingi hulitumia katima
majadiliano ya kibiashara.
“Vizuri, sasa Martin nimekuita hapa kuna
jambo moja nataka kuongea na wewe…Umefanya kazi kwa muda wa miaka 10 sasa,
tangu umekuja nimeona mafanikio makubwa sana katika kampuni yangu, nimepata
faida kubwa ya kifedha lakini pia kuwa na wateja wengi hadi kampuni inazidiwa,
yote hii ni kwa ajili ya ufanisi wako wa kazi iliotukuka ambao umewaambukiza
hata wafanyakazi wengine, Asante sana Martin!” Bosi wake Martin alimshukuru
Martin.
“Asante bosi wangu, sehemu hiyo ni sehemu
tu ya utendaji kazi wangu na utekelezaji wa majukumu yangu.” Alijibu Martin
huku akitabasamu. Kwake yeye pongezi na shukrani alizizoea sana ila siku hiyo
ilikuwa tofauti na yeye aligundua hulo. Alihisi pengine anapandishwa cheo,
“Sasa, kutokana na utumishi wako
uliotukuka, nimeonelea nikupatie kitu kidogo kama sehemu ya shukrani yangu
kwako…” Bosi wake Martin alitoa hundi aliyoitayarisha kwa muda mrefu.
“Bosi…..” Martin hakuamini alichokiona,
ilikuwa ni hundi ya dola za kimarekani milioni moja na nusu (USD 1,500,
000).
“Ndiyo Martin umeiheshinisha kampuni
yangu, nami nakuzawadia kiasi hicho cha fedha kama mtaji wa kuanzia,
katengeneze biashara yako mwenyewe, nataka nikuone ukitumia uwezo wako na
kipaji Mungu alichokujalia kutimiza ndoto zako.” Boss alimueleza Martin.
Kwa furaha aliyokuwa nayo Martin
alishindwa kujizuia, alilia kwa furaha aliyokuwa nayo, hakuamini kile
kinachomtokea.
Martin akafungua kampuni yake ndogo ya
ujenzi na Kutokana na bidii yake ya kazi, uaminifu na kumaliza kazi kwa wakati,
alipata tenda nyingi sana za watu binafsi, makampuni na hata kujenga miradi
mbalimbali ya kiserikali. Miaka mitano baadae alikuwa amefanikiwa kwa kiasi
kikubwa na kampuni yake ilikuwa inajulikana sana. Miezi michache baadae
alikutana na binti aitwaye Annabelle Ike, walipendana na kisha kufunga ndoa na
mwaka mmoja baadae wakapata mtoto wa kike waliyemuita Ritha.
Wakati wote waliishi kwa furaha sana,
Martin aliipenda familia yake sana na alifanya kila aliloweza kuhalikisha kuwa
wakati wote anatimiza majukumu yake kama mume na baba katika familia yake.
Ritha alifika umri wa kwenda shule, Martin
alibeba jukumu la kuhakikisha kuwa binti yao anapata elimu bora. Pamoja na kazi
nyingi alizokuwa nazo Martin, kamwe hakuacha kutenga muda wa kukaa binti yake
kumsaidia kazi za shule kuongea naye ili kujua anakutana na changamoto gani.
Ninabell mke wa Martin na mama wa Ritha,
siku zote alijiona ni kama amepewa upendeleo kuwa na mwanaume kama Martin.
Ritha alikuwa akifanya vizuri sana shuleni, Martin alijivunia sana kuwa na
binti huyo. Ritha alianza sekondari kidato cha kwanza ufaulu wake kama
ilivyokuwa shule ya msingi. Alipofika kidato cha 2 alifanya mtihani wa taifa
uliokuwa kipimo cha kwenda kidato cha tatu, Ritha alifanya vizuri sana.
Alimpelekea matokeo baba yake, Mr. Martin ambaye alifutahishwa sana na matokeo
yale, “Ooh! My Angel, ninajivunia sana wewe binti yangu…..Una A ngapi….1, 2, 3,
4, 5, 6…Dah! Am proud of you my Angel” Martin alimpingeza mwanaye.
“Am proud of you too dady…” Ritha
alimwambia baba yake kwa sauti ya kudeka
“Umemuonesha mama yako?” Martin alimuuliza
mwaye kama kamuonesha matokeo yale mama yake.
“Hapana baba, yuko chumbani kwake…” Ritha
alijibu huku akichukua matokeo yake kwa baba yake.
“Okey nenda kamuoneshe mama atafurahi
sana.”
“Asante baba…” Ritha akajibu kisha akaanza
kupiga hatua kuelekea chumbani kwa mama yake, mara akakumbuka kitu.
“Baba leo utanipeleka cinema?” Ritha
alimuuliza baba yake ikiwa ni ahadi aliyopewa na baba yake kabla hajafanya
mtihani wa taifa.
“Oooh! Yeah lazima twende na umwambie mama
yako leo ajiandae leo usiku tutakwenda Cinema kuna filamu mpya ya Ken Eric na
Yul Edochie waigizaji mnaowapenda”
“Asante baba, nakupenda”
“Nakupenda pia mwanangu” Martin naye
alijibu na kumuacha binti yake aende kwa mama yake.
Martin alimuwekea utaratibu binti yake
kuwa endapo anataka vitu vya kujifurahisha ni lazima avifanyie kazi, hawezi
kuvipata bure tu. Hivyo ndivyo ilivyotekea kabla hajafanya mtihani, Ritha
alimuomba baba yake ampeleke kwenye Cinema lakini baba yake alimwambia kuwa
utaratibu ni ule ule, nilazima afaulu mtihani kwake ndipo anpekeke Cinema.
Utaratibu huu ulimsaidia sana Ritha kufanya vizuri shuleni kwani alijua
kwakufanya hivyo basi angepata chochote anachotaka bila maswali.
Alipofika kidato cha tatu alipata likizo
ya katikati ya mwaka yaani nusu muhula ambapo awali aliahidiwa akifaulu basi
atapelekwa kijijini kupumzika na babu na bibi yake jambo ambalo Ritha alikuwa
analisubiria sana.
Siku ya safari iliwadia, na siku hiyo
ilikuwa ni mwisho wa wiki yaani jumamosi, walidamka asubuhi na mapema kila
mmoja akajiandaa kwa ajili ya safari. Waliingia ndani ya gari yao na kuanza
safari kuelekea kijijini kwao.
_____________
Usikose Sehemu ya 2 ya Hadithi hii.
0 Comments