MJUE HASEENA PARKER MALKIA WA UHALIFU ALIYETIKISA MUMBAI

HASEENA PARKER


Pengine uliwahi kusikia ama uliwahi kuona filamu kuhusu mwamba huyu kutoka India aitwaye Haseena Parker, kama hukuwahi kusikia au kuona, usiwe na shaka leo unatoma simulizi kumuhusu mwanamama huyu amabaye alitikisa mji wa Mumbai. Haseena Parker aliingia moja kwa moja katika biashara haramu na magenge ya kihalifu baada ya mumewe Ibrahim Parkar kupigwa risasi mnamo Mwaka 1991 na jamaa aliyeitwa Arun Gawli akishirikiana na genge lake. Baadae yalitokea mauaji katika hospitali ya JJ, Shambulio hili la mauaji lilipangwa na kutekelezwa na Dawood Ibrahim kaka wa Haseena kulipiza kisasi baada ya kifo cha shemeji yake.

Haseena Parker akiwa kwenye sherehe

Baada ya kifo cha mumewe, Haseena alihamia kwenye kasiri lake jipya, liitwalo Gordon Hall Apartments huko Nagpada na huko ndiko alikuwa akiendesha shughuli zake za kihalifu. Aliipenda nyumba sana nyumba hiyo na ndipo alipoivunja na kuijenga upya na hakuna hata mmoja aliyethubutu kulalamika.

Haseena alikuwa na ushawishi mkubwa sana nchini India kiasi kwamba akawa anahusika katika masuala mbalimbali na kuwa kama daraja la makampuni ya ujenzi ambayo aliyasaidia kupata vibali mbalimbali vya ujenzi wa makazi hasa katika maeneo ambayo yalikaliwa na watu maskini chini ya miradi ya SRA. Parkar pia alihusika katika kujadili kuhusu haki miliki za filamu za Bollywood, haswa filamu zilizokuwa zinakwenda kuuzwa Urusi ya Kati na nchi za Ghuba.

Dawood Ibrahim kaka wa Haseena Parker

Haseena Parkar alizaliwa katika wilaya ya Ratnagiri, Maharashtra katika familia ya Kiislamu ya Marathi. Baba yake Ibrahim Kaskar alikuwa mkuu wa polisi katika Idara ya Polisi ya Mumbai na mama yake Amina Bi, alikuwa mama wa nyumbani. Haseena Parkar alikuwa mdogo wake Dawood Ibrahim. Katika jumla ya watoto 12 wa Bwana Ibrahim, Haseena alikuwa mtoto wa saba na Dawood Ibrahim alikuwa mtoto wa tatu.

Mara tu baada ya Dawood ambaye alikuwa ni kaka yake na mkuu wa magenge ya kihalifu kukimbilia Dubai, Haseena alifuata nyayo za kaka yake huyo na kuingia katika ulimwengu wa uhalifu. Aliwaeleza  polisi na mahakama kwamba hakuwa akiwasiliana na kaka yake Dawood Ibrahim lakini baadae yeye ndiye alichukua biashara za kaka yake katika jiji la Mumbai na kuzisimamia kwa niaba yake. Vyanzo mbalimbali vinadai kuwa mwanamama huyu alikuwa na utajiri wa 5000 Crores.  kila Crore 1 inawakilisha milioni 10 piga hesabu hapo ujue ni mali kiasi gani alizokuwa anamiliki mwanamama huyu na hizo ni mali ambazo serikali haikuwa inafahamu.

Haseena alipoteza mwanawe mkubwa aliyeitwa Danish katika ajali ya barabarani mnamo 2006 kwenye barabara kuu ya Mumbai-Goa alipokuwa akirejea kutoka mjini Goa. Danish alikuwa akipendwa sana na mjomba wake, Dawood.

Kutokana na shughuli zake, Haseena ndiye mwanafamilia ya Dawood Ibrahim aliyefuatiliwa sana na polisi kupita mwanafamilia yeyote, na kila mara alikuwa kwenye macho ya polisi wakimfuatilia hatua kwa hatua. Alikuwa na kesi zaidi ya 88 kwa mkupuo ndani ya mahakama ambazo zote zilimhusisha yeye .

Pasipoti ya Haseena yenye No A2745364 iliyotolewa Aprili 5, 1997, ilikuwa halali hadi Aprili 6, 2007. Hata hivyo, Februari 14, 2005, baada ya kutembelea Mumbai Crime Branch ( MCB) baada ya kualikwa kwa mahojiano, pasi hiyo ya kusafiria ilifutwa. Alipotuma ombi la kupata pasi mpya, alinyimwa pasipoti hiyo kutokana na shughuli zake za uhalifu na uhusiano mkubwa aliokuwa nao na kaka yake, Dawood Ibrahim.

Mnamo Julai 6, 2014, Haseena Parker alifariki baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo, akiwa na umri wa miaka 55. Taarifa zinadai wakati umauti unamkuta alikuwa akifunga kwa ajili ya Ramzan. Haseena aliacha watoto watatu, binti wawili na wakiume mmoja.

Cover ya filamu ya HASEENA

 Maisha yake, na historia yake mwanamama huyu aliyewasumbua Polisi wa Mumbai imehifadhiwa katika filamu iliyoshirikisha mastaa kibao kama vile; 



Post a Comment

0 Comments