Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Betway Insider, unaeleza
kuwa wapenzi wa filamu za kutisha hupenda kuchagua kutazama filamu hizo hasa
majira ya jioni kama wanataka kupata usingizi mzuri. Matokeo ya utafiti yameonesha
kuwa kutazama filamu za kutisha kumeorodheshwa kama chaguo la mwisho
kulinganisha na kusoma vitabu na kusikiliza muziki. Utafiti huo pia umeonya
kuwa, kama unataka kupata usingizi mzuri usio na bughuza, usio na maruerue wala
mang’amung’amu basi usitazame filamu za kutisha, usiku.
Kutazama filamu za kutisha kunaweza kukusababishia
ubora wa usingizi wa 65% tu na kila unapostuka usiku utatumia dakika 26 hadi 30
kupata tena usingizi na hutaweza kufikia yale masaa 8 yanayopendekezwa na
wataalamu kuyatumia kwa ajili ya kulala usiku.
Pasi na shaka kuna baadhi ya watu watakataa
kukubaliana na utafiti huu kwakuwa wao wamezoea na wanapendelea kutazama filamu
za kutisha na kuogofya kuliko filamu nyingine. Kwa wale wasioweza kustahimili
kutazama filamu za kutisha basi mnashauriwa kutazama fimu nyingine kama za
kuchekesha nk hasa nyakati za usiku.
Vipi wewe, unaweza kutazama filamu ya kutisha usiku?
--------
Kama bado hujasoma hadithi ya CHUKIZO, usiwe na shaka
kwa kuwa ipo njia rahisi zaidi ya kutumia kuipata hadithi hii.
Unachotakiwa kufanya ni kulipia shilingi 3,000/=
kwenye M-PESA LIPA NAMBA 5359703 GEOFREY DISMAS MFIKWA (Kutoka mitandao yote).
Hatua ya pili ni kutuma risiti ya muamala wako kwenye
namba hii ya WhatsApp: 0768465103 Ukiweka Caption: CHUKIZO kisha subiri nakala
yako ambayo itatumwa njia ya WhatsApp.
_____
Kama una swali au maoni niandikie kwenye comment hapa
chini nami nitajibu swali lako na kufanyia kazi ushauri wako.
0 Comments